HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 15 September 2017

Watuhumiwa wa Madini ya Almasi yaliyokamatwa Uwanja wa Ndege wa JNIA wapandishwa kizimbani leo

 Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

Mkurugenzi wa Tathmini, Archard Alphonce Kalugendo (49) na Mthamini wa Madini ya Almas wa Serikali, Edward Joseph Rweyemamu (50) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la uhujumu uchumi na  kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya bilioni mbili.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka leo na wakili wa Serikali, Paul Kadushi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage. Imedaiwa kuwa Kalugendo ambaye ni Mkazi wa Kinyerezi na Rweyemamu anayeishi Mwananyamala ni waajiriwa wa Wizara ya Nishati na  Madini ambapo kati ya Agosti 25 na 31, mwaka huu, katika maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam na Shinyanga washtakiwa walitenda kosa hilo.
Imedaiwa kuwa, washtakiwa hao kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathamini walioajiliwa na Wizara ya Nishati na Madini waliisababishia serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania hasara ya USD 1,118,291.43 Ambayo ni sawa na 2,486,396,982.54.

Hata hivyo baada ya kusomewa shtaka hilo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu au DPP awasilishe hati ya kuipa mahakama hiyo kibali cha kuendesha kesi hiyo.

Upande wa mashtaka umedai kuwa upelezi bado haujakamilika na Hakimu Mwijage aliwaeleza washtakiwa hao kuhusu dhamana Mawakili wao wafuatilie Mahakama Kuu.

Kwa upande wa Wakili  Ludovico Nickson anayemtetea mshtakiwa Kalugendo ameomba upelezi ukamilike haraka na wataenda mahakama kuu kuomba dhamana
Wakili wa mshtakiwa Rweyemamu, Nehemiah Nkoko naye aliongeza kuwa washtakiwa wamekaa polisi kwa takribani wiki mbili anadhani upelelezi utakuwa umekwisha kamilika kwa kiasi kwa kuwa na kwamba bado kidogo sana.

Akijibu kuhusu upelelezi, Kadushi amedai watahakikisha wanakamilisha upelelezi kwa wakati.

Kesi itatajwa Septemba 29, mwak huu, washtakiwa wamepelekwa rumande.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad