HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 4 September 2017

WATOTO WA KIKE ELFU 3329 WALIOPANGIWA KUKEKETWA WILAYANI SENGEREMA MKOANI MARA WAOKOLEWA.

Watoto wa kike elfu tatu, mia tatu ishirini na tisa kati ya watoto elfu tano mia sita sitini na wawili waliopangiwa kukeketwa katika msimu wa ukeketaji wa mwaka 2016 katika wilaya ya Serengeti mkoani Mara,waliokolewa kufanyiwa ukatili huo baada ya Kanisa la Anglikana doyosisi ya Mara kujenga  kituo maalum cha kuwahifadhi baada ya kukataa kukeketwa na kuzikimbia familia zao.

Akizungumza wakati wa kikao cha Bodi ya  kituo hicho kinachojulikana kama Nyumba Salama, Meneja wa Shirika la Utafiti na Tiba Barani Afrika-AMREF wilaya ya Serengeti Bwana GODFREY MATUMU amesema utafiti uliofanywa wilayani humo umebaini kuwa katika msimu huo wa ukeketaji, baadhi ya wazazi waliwakeketa watoto elfu mbili, mia tatu thelathini na watatu nyakati za usiku na wengine walifanyiwa ukatili huo baada ya kufichwa katika wilaya ya Tarime na nchi jirani ya Kenya.
Hata hivyo, pamoja na mafanikio hayo ya Nyumba Salama ya kuwakoa watoto wa kike na vitendo hivyo vya  ukatili dhidi ya ukeketaji, mgogoro mkubwa wa uendeshaji wa kituo hicho umeibuka,hali ambayo imesababisha Askofu wa Kanisa la Anglikana dayosisi ya Mara Dakta GEORGE OKOTH kuwafukuza kazi baadhi ya walikuwawatumishi wa kituo hicho.

Chanzo: ITV Tanzania

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad