HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 16 September 2017

WANASOKA, WACHEZAJI WA ZAMANI WAUNGANA KATIKA KAMPENI YA UZALENDO KWANZA

Mwenyekiti wa Kampeni ya UZALENDO KWANZA, Steven Mengele almaarufu kwa jina la kisanii Steven Nyerere, akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar wakati wakiwatambulisha wanachama wapya ikiwemo wasanii wa filamu wa zamani pamoja na wachezaji mpira tukio lililoendana na kutoa msaada kwa wazalendo waliopata matatizo wakati wakitumikia taifa la Tanzania. Pichani kushoto ni Msanii wa Filamu Misayo Ndumbagwe. PICHA ZOTE NA KAJUNASON/MMG.

Wanachama wa UZALENDO KWANZA wakifuatilia kwa makini tukio.
Mwenyekiti wa Kampeni ya UZALENDO KWANZA, Steven Mengele almaarufu kwa jina la kisanii Steven Nyerere, akiongea wakati akimkabidhi msaada wa fedha na matumizi ya nyumbani mwandishi mpiga picha wa zamani, Athuman Hamis ambaye ni mzalendo aliyepata ajali na kumsababishia ulemavu kwa miaka 10 sasa amekuwa akitembea kwenye kiti.
Mwandishi mpiga picha wa zamani, Athuman Hamis akitoa shukarani zake kwa watu wote walioweza kujichanga na kumpatia msaada.
Mwenyekiti wa Kampeni ya UZALENDO KWANZA, Steven Mengele almaarufu kwa jina la kisanii Steven Nyerere, akimkabidhi kitu cha kutembelea, Rajabu Shabani ambaye ni mlemavu wa miguu.
Mwanasoma wa zamani akiongea wakati wa kujiunga na kampeni ya UZALENDO KWANZA.
Msanii Hellen George 'Ruby' akiimba kidogo wimbo wa UZALENDO KWANZA.
Wasanii wa zamani waliojiunga na kampeni ya UZALENDO KWANZA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad