HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 15, 2017

WANANCHI WA KILOLO MKOANI IRINGA WAJITOKEZA KWA WINGI KUJISAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA

Zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa limeendelea mkoani Iringa ambapo mara hii linafanyika katika Wilaya ya Kilolo Kata za Kimala, Idete na Dabaga.
Kwa mujibu wa Afisa Usajili wa Wilaya hiyo Ndugu Kelfasi Walingozi utaratibu unaotumika ni wa kuwasajili Wananchi kwa Kata ambapo kwa kushirikiana na Viongozi wa Wilaya, Kata, Mitaa na Vijiji. Amesema mpaka sasa zoezi limeanza vizuri na mwitikio wa watu ni mkubwa sana.
“ Kwakweli umuhimu wa Vitambulisho vya Taifa ni mkubwa kwa wananchi na wananchi wanatambua umuhimu wake ndiyo maana unaona wazee hawa wanajihimu kufika kwenye vituo kusajiliwa” Alisema 
Mkoa wa Iringa uko kwenye Wilaya ya mwisho kukamilisha usajili Vitambulisho vya taifa ambapo Wilaya zingine za Mufindi na Iringa tayari zilishakamilisha zoezi hilo na wananchi kwa sasa wanasubiri kukabidhiwa Vitambulisho vyao.
Wakazi wa Kijiji cha Itonya wakiwa wamekusanyika kwenye kituo cha Usajili kilichopo Wilaya ya Kilolo mkoa wa Lindi. Mbali na kujaza fomu za maombi ya Vitambulisho wakazi hao pia wanachukuliwa alama alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki.

Hawa ni baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kimala Kata ya Kimala wakiwa wamejumuika na baadhi ya wazee kupata huduma ya Usajili wakati zoezi la kuwasajili likiendelea kijijini hapo.  
Mkazi wa Kijiji cha Uluti Kata ya Kimala akiweka alama za vidole kwenye mashine ya kuchukua alama za kibaiolojia wakati wa Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kijijini hapo. 
Kinamama wakikamilisha zoezi la Usajili linaloendelea katika Kijiji cha Uluti. Mpango wa Usajili katika Kijiji hicho umezingatia utaratibu wa kutoa kipaumbele kwa kina mama na watoto, wazee na wajawazito wanaofika kijijini hapo kupata huduma ya usajili. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad