HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 15 September 2017

SESEA yahitimisha mufunzo ya kitaalamu Halmashauri ya kilwa .

Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.
Mradi wa kuimarisha  mifumo ya elimu   katika nchi za Afrika mashariki  (SESEA)  ambazo ni Tanzania, Kenya na Uganda imehitimisha mafunzo yake kupitia chuo kikuu cha  Agha Khan katika wilaya ya Kilwa  mkoani Lindi.
Hafla hiyo iliofanyika katika Halmashauri ya Kilwa mkoani Lindi ambao mradi huo unoafadhiliwa  na Global Affairs Cannada pamoja na Agha Khan Foundation unaolenga kuongeza  taaluma  kwa walimu wa shule za awali  na za msingi  ili kufikia idadi kubwa ya wasomi nchini.
Akizungumza  Mkurugenzi wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu, Sayansi, teknolojia na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia Temu katika  hafla hiyo ya kuhitimisha mafunzo hayo  amesema kuwa   ushirikishwaji  kwa wazazi na  jamii kwa njia ya warsha  na semina  umesaidia kuongeza ushiriki katika  kusaidia  kuleta matokeo chanya  ya elimu kwa watoto wa kike na wa kiume  na imesaidia  kuweza kutunga vitabu vya hadithi  kwa lugha ya Kiswahili, na kiingereza   na kaika nukta nundu kwa kuzingatia mazingira yao.
Hata hivyo  Slyvia Temu amesema kuwa  kupitia mbinu ya Education Community of Practice mradi umeshirikiana na Halmashauri  kuanzaisha jumuiya za kitaaluma  za walimu 1,200 kwenye shule zote 150, jumuiya hizi huwai hukutana shuleni na kwenye klasta zao kuimarisha utaalamu wa kufundishia mbinu mpya ya kusoma kwa kujifunza (Reading to learn) ikiwa miongoni mwa walimu zaidi 750 waliopata mafunzo  hayo  na mradi uliwaongezea maarifa walimu 307 wanaume wakiwa ni 179 na wanawake ni  128 ili kuwafanya walimu wawe imara zaidi.
Nae  mwakilishi wa mkuu wa chuo cha Agakhan, Mkurugenzi wa mradi  Nicolaus Washira  amesema kuwa SESEA  lengo lake ni kutaka kuinua  na kuimarisha Elimu nchini pamoja na  kuongeza wigo la wasomi  kwa kutembelea wilaya 4 ambazo ni Klwa, Nachingwea, Newala pamoja na Lindi Vijijni.
Vilevile Mkurugenzi wa mradi, Bernard Orimbo amesema kuwa ;bila kupata Elimu  huwezi kupata maendeleo na ili nchi iweze kupata  mafanikio  huwezi kutumia bunduki bali elimu ndio hupaswa kuwa stari wa mbele; amesema Mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu, Sayansi, teknolojia na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia Temu  akizungumza na walimu wa Shule za msingi  ambapo walimu walifanya maonesho ya zana  za vitendo ambazo hutumika katika kufundishia  wanafunzi pindi wanapokuwa masomoni katika Halmashauri ya Kilwa mkoani Lindi. Profesa Slyvia Temu alimwakilisha  wa Katibu mkuu Wizara elimu, sayansi na teknolojia,  Dkt Leonard  Akwilapo.
Wanafunzi wa Shule za msingi  waliojitokeza katika hafla hiyo wakisikiliza namna jinsi SESEA inavyotoa huduma ya  Elimu na umuhimu wake katika Halmashauri ya Kilwa  mkoani Lindi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad