HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 14, 2017

WANAFUNZI 1000 WAPELEKWA NA GLOBAL LINK KWENDA KUSOMA VYUO VIKUU VYA NCHINI.


 Afisa wa Digitali wa Global Education Link (GEL), Micky Mussa akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akiwapeleka wanafunzi 100 kwenda kusoma katika vyuo vikuu vya nchini India.
 Mkurugenzi wa Udahili wa Global Education Link (GEL), Zakia Hussein akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akiwapeleka wanafunzi 100 kwenda kusoma katika vyuo vikuu vya nchini India.


Maafisa wa Global Education Link wakikagua nyaraka kwa wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya nchini India leo jijini Dar es Salaam.

MKURUGENZI wa Udahili wa Global Education Link (GEL), Zakia Hussein amesema kuwa wanafunzi wanaokwenda kusoma wanaangaliwa kwa ukaribu na Global hadi wanapohitimu ili kuweza kumsaidia mzazi kuona thamani ya fedha ya kumsomesha nje ya nchi.

Zakia aliyasema hayo wakati akiwapeleka wanafunzi 100 kwenda kusoma vyuo vikuu vya nchini India ambao wamepitia Global Education Link (GEL), amesema kuwa Global inafanya kila kitu kwa mwanafunzi anayepitia hapo wanaangaliwa kwa ukaribu tangu hatua ya awali hadi mwisho anapohitimu.

Amesema kuwa Global ni wakala mkubwa wa kupeleka wanafunzi nje ya nchi na imeweza  kujingea uwezo katika kufanya uwakala kwa wanafunzi kushindwa kupata vikwanzo vya kusoma nje ya nchi.

Zakia amesema kuwa wakati wa kupeleka wanafunzi ni lazima kwenda watendaji wa Global kwa ajili ya kuangalia makazi ya wanafunzi pindi wanaposoma katika vyuo mbalimbali.

Aidha amesema wanaendelea kupeleka wanafunzi awamu kwa awamu na pamoja na kudahili wanafunzi wapya katika ofisi mbalimbali za global za Dar es Salaam (Viwanja vya Sabasaba ), Arusha, Mwanza, Dodoma pamoja na nchi jirani za Zambia na Malawi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad