HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 7, 2017

WALIOTANJWA KWENYE RIPOTI YA MADINI YA ALMAS NA TANZANITE WATUPISHE - RAIS MAGUFULI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo Septemba 7, 2017 amepokea ripoti za uchunguzi wa madini ya Tanzanite na Almasi kutoka kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, zilizotokana na kamati mbili (Kamati ya Tanzanite iliongozwa na Mwenyekiti Dotto Biteko na Kamati ya Almas ilikuwa chini ya Mwenyekiti Mussa Azzan Zungu) zilizoundwa na spika wa Bunge, Job Ndugai . Muda mfupi baada ya kupokea ripoti hizo, Rais Dkt. Magufuli alisema kuwa ametengua uteuzi wa wateule wote waliotajwa katika ripoti hizo.
Miongoni mwa wateule wa Rais waliotajwa katika ripoti hiyo ni pamoja na Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Edwin Ngonyani. Wengine waliotajwa katika taarifa hizo ni pamoja na Katibu Tawala Eliakim Maswi, wabunge Willium Ngeleja na Andrew Chenge.

Katika hotuba yake aliyoitoa baada ya kupikea ripoti hiyo, Rais Dkt. Magufuli alisema "uwe RC,Waziri wau Mkurugenzi na umetajwa kwenye ripoti ya uchunguzi hauwezi kuendelea na wewe upo kwenye Serikali, Utupishe".

"Kuna baadhi ya wabunge kama ulivyosema mheshimiwa Spika, kila mahali yupo, katika kashfa fulani yupo, katika hili yupo, katika lile yupo. Tena wengine bado wapo bungeni na wakati mwingine wanachangia mpaka mishipa inawatoka, taratibu zifanyike kuwachukulia hatua" Rais Magufuli Rais Magufuli amewasifu watanzania wazalendo ambao wako tayari kutoa uhai wao kwa ajili ya Taifa lao.

"Tunawatumia watanzania wazalendo kupata taarifa za kizalendo kwa Taifa letu, wapo watanzania wanaorubuniwa na kuisaliti nchi yao, hao hawafai" Rais Dk John Pombe Magufuli, Ikulu. Dar es Salaam.

Katika maelezo yake kabla ya kumkabidhi Rais ripoti hizo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kwa muda mrefu watanzania wamekuwa wakilalamika serikali kutowajali na kuwasikiliza. Amesema kupitia serikali ya Awamu ya Tano sasa watanzania wote watakuwa na haki sawa na wote watasikilizwa.

"Watanzania ambao kwa miaka mingi wamejihisi hawasikilizwi na hawahurumiwi sasa ni wakati wao kujihisi kuwa ni watanzania na wanastahili haki zote kama watanzania kupitia serikali yako mheshimiwa Rais" Kassim Majaliwa

Rais Magufuli amemkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kwa ripoti hizo za madini kwa ajili ya kufanyiwa kazi mara moja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad