HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 19, 2017

Walimu wa jiji la Dar es Saaam kujengewa nyumba za kisasa.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amezindua rasmi wa Ufyatuaji wa Matofali kwaajili ya ujenzi wa ofisi za kisasa 402 za Walimu ambapo amewasihi Wadau na Wananchi kuunga Mkono jitiada hizo.
Katika uzinduzi huo  RC Makonda ameshiriki zoezi la Ufyatuaji wa Matofali kwaajili ya Ujenzi huo.

Makonda amesema lengo la Ujenzi wa Ofisi hizo ni kuboresha Mazingira ya kufanya kazi kwa walimu ili waweze kutoa Elimu bora kwa Wanafunzi na kuongeza ufaulu.

Amesema wapo wengi waliopanga kufanya ujenzi wa Ofisi za Walimu lakini mipango hiyo iliishia kubaki kwenye makarabrasha maofisini lakini kupitia juhudi zake na Kamati aliyoiunda wameweza kuleta matokeo chanya.
RC Makonda ametoa wito kwa Wananchi na Wadau kuchangia Mabati, Saruji, Kokoto,Mchanga, Nondo au Nguvu kazi ilikuwawezesha walimu kufanyakazi katika mazingira bora.

Amesema ataki kuona kwenye Mkoa wake Walimu  wanadhalilika kwa kukosa Ofisi na Vyoo hali inayopelekea kujisaidia kwa Majirani,Bar au Vichakani.

Aidha amesema hadi sasa amefanikiwa kupata mifuko zaidi ya 10,000 ya Saruji Mashine za kufyatulia Matofali,Gurdoza na vifaa vingine ambapo ataendelea kugonga hodi kwa Wadau ili waweze kuchangia ujenzi huo.
Amewaomba Wananchi kuwa na uzalendo kwa kujitoa katika ujenzi huo iwe kwa mtu binafsi au Vikundi vya Joaging,Timu za Mpira na vikundi vya maendeleo.

Ameipongeza Kamati ya ujenzi wa Ofisi za walimu,JKT,Jeshi la Magereza, Jeshi la Polisi,NHC, TBA,Channel Ten na Umoja wa Wamiliki wa Malori na wengine kwa namna wanavyojitoa kusaidia katika zoezi hilo.

Katika hatua nyingine RC Makonda amesema atatoa TV 30 kwa Magereza ya Ukonga, Segerea na Keko ili wafungwa wapate fursa za kutazama hotuba za Rais Dk. John Pombe Magufuli ili wajue maendeleo yanayofanyika uraiani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu Canal Charles Mbuge amesema hadi sasa kiasi cha fedha kilichotumika ni zaidi ya Million 200 ambapo watahakikisha ujenzi huo unakamilika.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu Kanali Charles Mbuge akizungumza katika uzinduzi wa ufyatuaji tofali za ujenzi wa ofisi za shule katika mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizugumza leo katika  uzinduzi wa  Ufyatuaji wa Matofali kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Shule   katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akishiriki wa Ufyatuaji wa Matofali kwaajili ya ujenzi wa ofisi za kisasa 402 leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanel Massaka,Globu ya Jamii).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad