HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 27 September 2017

WAETHIPIA 31 WAINGIA NCHINI BILA KINYUME NA SHERIA.

 Wahamiaji 40 kutoka Ethiopia  wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salam leo na kukutwa na mashtaka ya kuingia nchini kinyume cha sheria bila ya kuwa na kibali.
 Wahamiaji haramu wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kuwasiri tukoka walipokuwa wamehifadhiwa. 
 Wahamiaji Haramu wakisubiri kusomewa mashtaka ya kuingia nchini kinyume cha sheria bila ya kuwa na kibali leo jijini Dar es Salaam Katika Mahaka ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Picha na Avila Kakingo,Blobu ya Jamii.

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii. 
WATANZANIA wawili, Ibrahim Abdallah dereva wa gari aina ya Nissan Civilian namba T 669 DJH na kondakta  Christopher Steven wamepandishwa katika kizimba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kusafirisha binadamu kimagendo ambao raia 31 wa Ethiopia.

Aidha raia hao 31 wa Ethiopia wamesomewa mashtaka matano ya kuingia nchini kinyume cha sheria bila ya kuwa na kibali.

Mwendesha mashtaka wakili wa serikali kutoka Uhamiaji Novatus Mlay amedai Septemba 25, mwaka huu, huko Tuangoma wilaya ya Temeke watanzania hao walikutwa wakiwasafirisha raia hao 31 wa Ethiopia  kimagendo na kuwaingiza nchini kwa nia ya kuwapitisha na kuwasaidia kutoka Tanzania kwenda Afrika Kusini.
Hata hivyo, watanzania hao wamekana kuhusika na kosa hilo na kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 11, mwaka huu huku upande wa mashtaka ukieleza mahakama kuwa upelelezi haujakamilika huku watuhumia hao 31 wa Ethiopia wakikubali mashtaka yote waliyosomewa na kesi iendelea Oktoba 11, 2017 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.

Wakati huo huo, watanzania  watatu akiwamo dereva wa kampuni ya Dangote Cement Ltd, Khalid Abdallah, Hussein Hamad Hassan na Jumanne Mtambo pamoja na wahamiaji nane raia wa Ethiopia wamesomewa mashtaka matano likiwemo shtaka la kusafirisha kimagendo binadamu na kuingia nchini kinyume cha sheria.

Wakili Mlay amedai mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa kuwa, wahamiaji Solomon Ertiso, Gazahegn Tiroro , Haire  Latso, Thadius Lilanso, Dawit Habtam, Deznet Godebo, Feraru Gurana na Elioj Akola, Septemba 20,2017 katika eneo la Kongowe Mbagala walikamatwa wakiingia nchini bila ya kuwa na kibali.

baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa hao wote walikubali kuyatenda  makosa hayo huku  watanzania hao ambao wanakabiliwa na tuhuma za kusafirisha binadamu wanao wanadaiwa kuwasafirisha kimagendo wahamiaji hao haramu.

Mlay alidai kuwa siku hiyo ya tukio ya Septemba 20, 2017  huko Mbagala Kongowe Khalid, Hussein  na Jumanne wakiwa raia wa Tanzania  walikutwa wakiwasafirisha wahamiaji hao haramu kimagendo.

Alidai kuwa raia hao watatu wa Tanzania waliwasafirisha  kimagendo wahamiaji hao haramu kwa kutumia gari yenye namba za usajili T 961 DKA mali ya kampuni ya Dangote Cement Ltd kwa kuwatoa Tanzania kwenda nchini Afrika Kusini.

Pia washtakiwa hao, kuwa siku hiyo walikutwa wakisaidia kuwasafirisha wahamiaji hao ambao ni raia wa Ethiopia kimagendo  kwa kuwaingiza ndani ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Watanzania hao wamekana tuhuma hizo na kesi hiyo itaendelea Octoba 10 kwa ajili ya kutajwa huku Octoba 11 Raia hao wa Ethiopia watasomewa maelezo awali baada ya kukubali kutenda makosa hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad