HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 25 September 2017

UKOSEFU WA ELIMU YA AFYA YA UZAZI WATAJWA CHANZO CHA MIMBA ZA UTOTONI.

Ukosefu wa elimu juu ya afya ya uzazi ni sababu mojawapo inayochangia kupatikana kwa mimba za utotoni kwa wasichana wa kati ya umri wa miaka tisa hadi kumi na saba, hali iliyopelekea mkoa wa Katavi kuwa na asilimia kubwa zaidi ya asilimia 45.1 ya mimba za utotoni, tofauti na wastani wa kitaifa ambao ni asilimia 19.
Akizungumza katika tamasha la kutoa elimu ya uzazi kwa vijana  ambao ndio waathirika wakuu wa mimba za utotoni,kaimu katibu tawala wa mkoa wa Katavi Bwana Wilbard Marandu amesema ili kupunguza mimba za utotoni mkoa kwa kushirikiana na wataalamu wa afya na mashirika mbalimbali unafanya jitihada za makusudi kupunguza hali hiyo.

Bwana Seif Katiko ni mratibu wa Marie Stopes mkoa wa Katavi, amesema wanakutana na changamoto mbalimbali zinazokwamisha utoaji elimu ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango.

Inaelezwa kuwa asilimia 10 ya wanafunzi wa shule za sekondari nchini wanapata mimba, huku asilimia 34 ikiwa ni ya wanafunzi wa shule za msingi na asilimia 52 ni ya watoto wasio mashuleni.

Chanzo: ITV Tanzania

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad