HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 14 September 2017

Uhamiaji yapata msaada wa vitendea kazi toka Shirika la IOM

 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala akipokea msaada wa vifaa mbalimbali uliotolewa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM. Anayekabidhi vifaa hivyo ni, Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Tanzania Dkt. Qassim Sufi. Vifaa hivyo vina jumuisha Kompyuta, mashine za kutolea nakala na kuchapishia vyenye thamani ya Dola za Kimarekani elfu arobaini. Tukio hilo ambalo lilishuhudiwa na wana habari nimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, Dar es Salaam.
  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala(kulia) pamoja na Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Tanzania Dkt. Qassim Sufi(kushoto) wakisaini nyaraka za makabidhiano ya msaada wa vifaa mbalimbali uliotolewa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM.
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala(kulia) akibadilishana nyaraka na  Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Tanzania Dkt. Qassim Sufi za makabidhiano ya msaada wa vifaa mbalimbali uliotolewa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM.
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala akizungumza wakati wa mamakabidhiano ya msaada wa vifaa mbalimbali uliotolewa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad