HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 13 September 2017

TIKETI ZA KWANZA ZA KOMBE LA DUNIA 2018 KUANZA KUUZWA ALHAMISI

Kuelekea michuano ya fainali ya kombe la dunia nchini Urusi hapo mwakani tayari tiketi za awali zinatarajiwa kuanza kuuzwa mnamo siku ya Alhamisi.


Mashabiki sasa wataweza kuwasilisha maombi yao kupitia tovuti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani ‘FIFA’ na tiketi zitauzwa kwa awamu mbili.
Bei za tiketi zinatarajiwa kuanza paundi 79 kwa mechi za mzunguko wa pili hadi kufikia paundi 829 katika mchezo wa mwisho.
Kwa mujibu wa sera za awali kuhusiana na upatikanaji wa tiketi hizo wakazi wa nchini Urusi watakuwa na bei yao maalum itakayo anzia na paundi 17.


Tiketi ya mwisho itakayokuwa na gharama kubwa zaidi Kombe la Dunia mwaka 2018 ni paundi 829 ambalo ni ongezeko la paundi 151 ukilinganisha na zile za fainali ya mwisho ya Rio de Janeiro nchini Brazil mwaka 2014.
“Tumeweka mfumo mzuri wa upatikanaji wa tiketi ambao utawezesha mashabiki wote kupata nafasi ya kuzipata,” amesema Katibu Mkuu wa Fifa, Fatma Samoura.
Maombi yote yaliyofanywa katika awamu ya kwanza, kabla ya Oktoba 12 mwaka 2017, yataingizwa katika waombaji wa jumla kama endapo tiketi hazitatosha kwa waombaji wote.
Matokeo ya waombaji wote yatatambuliwa maombi yao kuanzia Novemba 16 mwaka 2017.wakati ambapo tiketi zitatengwa kwa awamu ya kwanza.
Wakati awamu nyingine ikitarajiwa kuanza Desemba 5 baada ya kufanyika kwa hatua ya mchujo wakati michuano hiyo mikubwa na ya nayoshika nafasi ya kwanza katika mchezo huo yanatarajia kuanza kutimua vumbi Juni 14 wakati Urusi ikijitupa katika uwanaja wa Luzhniki huko Moscow.
Tayari nchi saba zimeshatafuta makazi Urusi kwa kufikia timu zao za taifa ambazo ni Brazili, Ubelgiji, Iran, Mexico, Japan, Saudi Arabia na Korea ya Kusini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad