HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 13 September 2017

TANZANITE WAKABIDHIWA BENDERA YA TAIFA,TAYARI KUWAKABILI NIGERIA SEPT 17

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Waizara ya Michezo, Yusuph Singo  akiwa anamkabidhi bendera ya taifa kwa nahodha wa timu ya wanawake chini ya miaka 20 Tanzanite Stars kuelekea nchini Nigeria kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kuwania kucheza Kombe la Dunia. katikati ni Kocha Mkuu wa timu hiyo Sebastian Mkoma na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Wilfred Kidau na baadhi ya viongozi wengine kutoka TFF.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Timu ya Taifa ya Wanawake wenye umri wa miaka 20 'Tanzanite Stars' leo imekabidhiwa bendera ya Taifa na Mkurugenzi wa Michezo kabla ya safari ya kuelekea Nigeria kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Ufaransa, 2019.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Waizara ya Michezo, Yusuph Singo amewakabidhi bendera ya taifa kwa timu hiyo  inayoondoka leo usiku kuelekea nchini Nigeria kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kuwania kucheza Kombe la Dunia.

Akiwakabidhi bendera mbele ya Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Wilfred Kidau, Singo amesema kuwa ana imani kubwa sana na kikosi cha wachezaji hao wanaoelekea nchini Nigeria na amewataka warejee nyumbani wakiwa kifua mbele na ushindi.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Waizara ya Michezo, Yusuph Singo akizungumza kabla ya kukabidhi bendera ya timu ya Taifa leo Jijini Dar es salaam , Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Wilfred Kidau, Mkurugenzi wa Ufundi Salum Madadi (kwanza kulia) na Mjumbe wa kamati ya Utendaji TFF Lameck Nyambaya.

"Wachezaji, mnapokwenda kule mnatakiwa mfahamu kuwa mna jukumu la kuipeperusha bendera tya Tanzania na kutuwakilisha Watanzania zaidi ya milioni 50 na hii ni  fursa kubwa kwa sola ketu kujitangaza  kimataifa kama mnavyoona siku hizi wachezaji wa Tanzania wameanza kuchukuliwa kwa wingi kwenda nje," alisema Singu.

Kocha wa Tanzanite, Sebastian Mkoma alitamba kuweza kuiondoa kwneye  mashindano timu ya Nigeria ambapo mchezo huo umepangwa kufanyika  17 mwaka huu na mshindi wa mchezo huo atakutana na Morocco.

"Tumejiandaa vizuri ingawa tulikosa mechi za kirafiki za kimataifa, tutahakikisha tunapata matokeo mazuri," alisema Mkoma
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Waizara ya Michezo, Yusuph Singo kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF na Kikosi cha Tanzanite Stars kinachotarajiwa kuondoka usiku wa leo kuelekea nchini Nigeria.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad