HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 14 September 2017

Tigo Business huduma mpya ya kuongeza ufanisi, ukuaji na faida kwa biashara nchini

Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali na uvumbuzi, Tigo Tanzania imetambulisha huduma mpya ya Tigo Business inayotoa bidhaa na huduma mahsusi kwa biashara na mashirika ya aina yote; ili kuongeza ufanisi, ukuaji na faida. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema Tigo Business inatoa huduma za kipekee zinazolenga mashirika ya umma, serikali, biashara binafsi, kampuni za usambazaji na usafirishaji, mashirika ya fedha, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, wachimbaji madini, viwanda na kadhalika; huku ikiwapa uhuru wa kufanya shughuli zao kwa ueledi zaidi na kuwawezesha kufanikisha miradi yao nchini na nje ya nchi. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya simu ya Tigo Tanzania, Simon Karikari akifafanua jambo wakati wa uzinduzi huo.

‘Tigo Business ndio huduma ya mawasiliano ya biashara inayokuwa kwa kasi zaidi nchini. Inajumuisha biashara za aina zote bila kutegemea ukubwa wa biashara au bajeti, huku ikiwapa wafanyabiashara amani na uhuru wa kushugulikia masuala ya muhimu zaidi yanayohusu ukuaji wa biashara zao,’ Karikari alisema.

Tigo Business itafanikisha mahitaji tofauti ya mawasilano ya biashara ikiwemo mawasiliano ya sauti, data na mifumo ya mitambo ya biashara kwa ufanisi wa juu na kwa gharama nafuu zaidi. Kwa kutumia uwekezaji mkubwa wa Tigo katika mkongo wa mawasiliano (fibre) na  kituo cha kuhifadhia kumbukumbu (data centre), Tigo business imejikita kuongoza soko la mawasiliano ya kisasa ya biashara huku ikiboresha jinsi wateja wanavyotumia mawasiliano ya kisasa kukuza biashara zao. 

‘Tigo Business inaelewa kuwa dunia ya sasa imeunganishwa kwa mtandao na hii inabadilisha jinsi biashara zinvyoendeshwa. Kwa kutumia mtandao wetu na bidhaa zetu,  Tigo inatumia uzoefu wetu wa maisha ya digitali kuleta mageuzi katika mifumo ya biashara,’ Karikari alisema.
Tigo Business, kauli mbiu yetu ni biashara yako ni biashara yetu.
Tigo Business ni ya kwanza kuletea ofa ya Business Day inayowapa wafanyabiashara muda wa maongezi na data kwenda mitandao yote bila kikomo, huduma ya simu nje ya nchi na huduma ya makundi maalum ya simu ambayo inawawezesha kupiga simu za biashara kwa bei nafuu zaidi huku wakiwa hewani kwa wakati wote.

Tigo Business pia inaongoza soko kwa kuwa na kituo cha kisasa zaidi cha kuhifadhia kumbukumbu (Tier 3 Designed Data Center) ya kwanza hapa nchini Tanzania, inayowahakikishia wateja kuwa watakuwa hewani 99.99% ya muda, huku wakiwa na uhakika wa ulinzi wa kisasa na utendaji wa hali ya juu wa mitambo yao. 

Tigo Business pia inatoa ofa ya Mtandao usiohamishika (Advanced Dedicated Fixed Internet) na Corporate Access Point Network Solutions (APN) ambazo zinaunganizha wafanyakazi, mitambo na mashine moja kwa moja kwa njia ya mtandao bila kuhitaji uangalizi wa binadamu. Corporate APN inawezesha wafanayabiasahra kufuatilia utendaji wa mifumo yao ya biashara na uwekezaji wao kwa muda wote na toka sehemu yoyote ile bila hitaji la wao kuwa ofisini. 

Tigo Business pia inatoa huduma bora kwa wateja, masaa 24 kupitia mfumo wetu maridhawa wa huduma kwa wateja. Tunajitatiti kuwa mshirika wako wa karibu katika biashara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad