HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 6 September 2017

TFF YAUNDA KAMATI YA TUZO ZA WACHEZAJI CHINI YA MSAFIRI MGOYI

 Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, Alfred Lucas


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeunda Kamati ya Tuzo za Wachezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, chini ya Mwenyekiti, Ahmed Iddi Mgoyi, maarufu kama Msafiri Mgoyi.

Katika Kamati hiyo, Makamu Mwenyekiti atakuwa Almasi Kasongo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Dar es Salaam, wakati Katibu Mkuu ni Amir Mhando, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu itakuwa inachagua wachezaji bora wa mwezi, goli  bora, mwamuzi bora, kocha, kipa bora na mchezaji bora wa msimu. 

Ahmed Iddi Mgoyi maarufu kama Msafiri Mgoyi ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo za Wachezaji Bora wa Ligi Kuu

Wajumbe wa Kamati hiyo ni Katibu Mkuu wa zamani wa Simba SC, Patrick Kahemele, Kocha wa zamani wa Yanga, Kenny Mwaisabula, mchezaji wa zamani wa kimataifa nchini, Said George na Waandishi wa Habari Ibrahim Masoud, Fatma Likwata, Salehe Ally, Gift Macha na Zena Chande.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad