HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 12 September 2017

TAKUKURU YAANZA KUCHUNGUZA WA FEDHA TADFAA.

Mhazini wa chama cha waigizaji Taifa (TADFAA), Lydia Mgaya akizungumza na mwandishi wa Michuzi blog jijini Dar es Salaam leo baada ya kumaliza kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Kuhusiana na Ubadhirifu wa fedha ndani ya  chama cha waigizaji Taifa (TADFAA).

Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii.
TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru), imeanza upelelezi kuhusiana na kiasi cha sh. Milioni tano fedha ambazo zilitolewa na mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF mwaka jana kwenda kwa  chama cha waigizaji Taifa (TADFAA) kwa ajili ya kuwahamasisha wasanii wote nchini kujiunga na mfuko huo na kunufaika na mambo mengi ikiwemo matibabu.

Upepelezi huo unafuatia taarifa iliyowasilishwa na mjumbe wa bodi na Mhazini wa chama hicho, Lydia Mgaya ambaye mapema leo amehojiwa na Takukuru, kwenda kwa Rais wao Simon Mwakifwamba mwaka huu, kufuatia hela hizo kutoonekana bila ya kujua zimetumikaje tangu zilipoingizwa katika akaunti ya chama hicho iliyopo  benki CRDB Februari mwaka jana.

Akizungumza na Michuzi blog leo, Lyidia amesema, “Nilipeleka barua katika shirikisho la filamu Tanzania (TAF), kulalamikia ubadhirifu wa fedha unaofanywa na mwenyekiti wetu, Elia Mjata na Katibu wake Twiza Mbaruku ambapo ziingie hazionekani zimeenda wapi na je kama zipo zinafanya nini, kama zipo ina maana hazina matumizi”.

Amesema, kuwa akiwa kama muhazini, alienda pamoja na Mwakifwamba katika benki hiyo tawi la millennium Tower ili kupata taarifa za akaunti (Bank statement) lakini ilishindikana baada ya kuambiwa kuwa, akaunti yao hiyo ina shilingi 28,000 tu na ili kupata taarifa za akaunti (Bank statement) lazima wawe na  shilingi 90,000/- ila walihakikishiwa kuwa fedha za PPF kweli ziliingia.

“Chama cha wasanii kimechafuka, wasanii wamechafuka, serikali na Wizara yetu haituamini tena, ili kurudisha heshima lazima tuanze kuwaondoa viongozi wote wabadhirifu wa fedha ili kurudisha chama katika hadhi yake tuweze kuaminika upya na tukipewa mradi wowote tuufanye kwa wakati”. Amesema Mgaya.

Aidha amewaasa watu ambao wanampango wa kuombea uongozi kwenye chama hicho na wanampango wa kuiba ni vema wakabadili mawazo na kufikiria zaidi kufanya mazuri ndani ya chama na kurudisha heshima.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad