HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 11 September 2017

Serikali yapokea vituo vya afya 26 vyenye thamani ya Zaidi ya Sh 2.5 b mkoani Kigoma

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amezindua majengo 26 ya kutolea huduma za Afya ya Uzazi katika Mkoa wa Kigoma.

Akitoa hutuba wakati wa uzinduzi wa moja ya  majengo hayo ya huduma za Afya za Uzazi, katika Zahanati ya Mwakizega iliyopo Wilayani Uvinza, Mkoani humo mapema jana Septemba 9,2017, Dk. Kigwangalla alipongeza wadau waliofanikisha ujenzi na ukarabati wa majengo hayo kwani yatasaidia kupunguza vifo vya akina Mama vitokanavyo na uzazi pamoja na kupanga uzazi ulio salama.

“Natoa shukrani zangu za dhati kwa wafadhili  wa mradi huu BloombergPhilanthropies na Foundation  H&b Agerup na Shirika la Engender Health pamoja na wataalamu wetu  kwa kusimamia kikamilifu ujenzi na ukarabati wa majengo haya hadi kukamilika, Natambua mmefanya kazi kubwa, kwa niaba ya Serikali na kwa niaba yangu binafsi, nasema asanteni sana” alieleza Dk. Kigwangalla.

Dk. Kigwangalla ameongeza kuwa, kwa hatua hiyo vifo vitokanavyo na uzazi vitapungua kwani havikubaliki ambapo alitoa wito kwa akina Mama kuwahi mapema Kliniki pindi wanapojihisi wajawazito, maana mama mjamzito anatakiwa kuanza kuhudhuria kiliniki pale ujauzito wake unapofikisha wiki 12.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa EngenderHealth Tanzania, Bi. Lulu Ng’wanakilala aliwashukuru wadau na Serikali kwa kushirikiana katika kufanikisha miradi hiyo hivyo aliahidi kuendelea kushirikiana katika kuokoa maisha ya akina mama hasa katika uzazi salama.

Bi. Lulu alieleza kuwa mradi huo umeweza kufanikisha majengo hayo 26 katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo wa Kigoma, ikiwemo maeneo ya katika Zahanati za Sigunga, Kelenge, Kazuramimba, Basanza (Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza). Rungwempya, Mutala, Bugaga, kitema, Muvinza, Kagerankanda na Makere (Wilaya ya Kasulu), Busunzu, Kumuhasha na Nyakasanda (Kibondo), Nyagwijima, Katanga,Nyabibuye, Kabingo na Kazilamihunda (Wilaya ya Kakonko).

Pia jengo lingine ni katika Zahanati ya Muhanga (Halmashauri ya Mji wa Kasulu) hivyo katika vituo vya  Songambele na Kitambuka (Wilaya ya Buhigwe) na Kagunga katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.

Naibu Mkurugenzi wa EngenderHealth, Lulu Ng’wanakilala akielezea kuhusu miradi ambayo imekuwa ikifadhiliwa na asasi anayoiongoza. Wakati asasi ya EngenderHealth ikikabidhi vituo vya afya 26 kwa serikali, hafla hiyo imefanyika katika kijiji cha Mwakizega, wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma
Mwakilishi wa Bloomberg Philanthropies Dkt. Godson Maro akiwasilisha salamu na kuelezea kuhusu asasi anayoiwakilisha.
Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mwanamvua Hoza Mlindoko akimkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Dkt. Hamis Kigwagala katika sherehe hiyo ya makabidhiano
Umati wa wanakijiji waliohudhuria hafla hiyo
Meza kuu wakiimba wimbo maarufu wa kabila la Kiha ‘ikidolidoli’.
Mgeni rasmi kwa kushirikiana na meza kuu wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa kwa vituo hivyo vya afya.
Mkunga muuguzi wa kituo cha Afya Mwakizega, Mary Twakazi (kushoto) akitoa maelezo kuhusu kitanda maalum cha kujifungulia kinamama kilichotolewa na shirika la EngenderHealth.
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na baadhi ya wafanyakazi wa mashirika wafadhili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad