HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 8, 2017

Serikali kupitia TCRA imetoa leseni kwa vituo 32 vya televisheni nchini.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipokuwa akijibu maswali leo Bubgeni Mjini Dodoma. (Picha na Daudi Manongi, MAELEZO, Dodoma)

Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma
 Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa leseni kwa vituo 32 vya televisheni hapa nchini ikiwa ni kuongeza muonekano na usiku katika maeneo mbalimbali  ya nchi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura leo Bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Martin Alexander Mtonda Msuha Mbunge wa Mbinga Vijijini ambapo alitaka kujua idadi ya vituo vinavyorusha matangazo kwa njia ya televisheni na Makampuni yanayomiliki vituo hivyo.

Aliongeza kwa kuvitaja vituo hivyo vya Televisheni vilivyosajiliwa nchini kuwa ni pamoja na Independent Television (ITV), Star Television Channel Ten Television, TBC 1, TBC 2, East Africa Television (EATV), Agape Television (ATV), C2C Television, Dar es Salaam Television (DTV), Abood Television, CTN Television, Capital Television, Clouds TV, VIASAT 1 Television, Sibuka Television, Sokoine University of Agriculture Television (SUATV) na Tumaini Television.

Vituo vingine ni Mlimani Television, Tanga City Council Television, Imaan Television, Morning Star TV, Africa Internet Television Ltd, Uhai Television Limited, Barmedas TV, Target Television, Tabibu Television, Africa Swahili Television, Cable and Satellite Consultancy Limited, WRM Television Network, Dira Television, Parliament Media Trust (Bunge TV), Mahaasin Television.

Aidha alifafanua kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) ndio yenye dhamana ya kutoa leseni ya maudhui ya utangazaji wa Televisheni za aina mbili ambazo ni Leseni za maudhui yanayotazamwa bila kulipia na maudhui ya Kulipia.

Alizidi kueleza kuwa leseni hizo zimegawanywa kimasoko ambapo kuna leseni za Kitaifa ambazo zinapaswa kuonekana nchi nzima na leseni za Kimkoa ambazo huruhusiwa kutangaza mikoa 10 ya Tanzania Bara, na leseni za kiwilaya ambazo huonekana Mkoa mmoja.

Mgawanyo huu wa kimasoko unatoa fursa kwa waombaji kutangaza maeneo wanayochagua kutokana na uwezo wao wa kifedha na kiundeshaji ambapo maudhui hayo ya bila kulipia yanapaswa kuonekana kupitia visimbuzi vya Makampuni ya Agape Associates Limited, Basic Transmission Limited na Star Media (Tanzania) Limited. Visimbuzi hivyo ni TING, STARTIMES, DIGITEK na CONTINENTAL.

Naibu Waziri Wambura amevitaja vituo vyenye leseni ya soko la Kitaifa kuwa ni TBC1, Channel Ten, East Africa Televisheni, Independent Televisheni, Star Televisheni, Clouds TV na Bunge TV wakati vituo vyenye soko la kimkoa ni TV Imaan, Agape TV (ATV) na TV1 na vituo vilivyobaki vina soko la kiwilaya.

Aidha, Kituo cha TBC1 ambacho ni kituo cha Umma kinapatikana bila malipo ya mwezi kwenye ving’amuzi vyote vya miundombinu iliyosimikwa ardhini na vile vinavyotumia mitambo ya satelaiti kama vile Azam TV, DSTV na Zuku.

Kituo cha TBC 1 kinalazimika kuonekana bila malipo kwa mujibu wa masharti ya leseni za makampuni ya miundombinu ya utangazaji ya ardhini (DTT) na Satellite (DTH).
                        
Kuhusu muonekano na wa TBC1 maeneo yote nchini, Naibu Waziri Wambura amesema kuwa Serikali kupitia Bunge la Bajeti ya mwaka 2017/2018 imetenga jumla ya Sh. Bilioni 3 ambazo ni fedha za miradi ili kuboresha muonekano wa matangazo ya TBC1 nchi nzima.   

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad