HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 15 September 2017

RC Rukwa: Kukamata na kuchoma nyavu haitoshi, tuwachome wahalifu”

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu, Zelote Stephen akitoa maelekezo namna ya kuziteketeza nyavu haramu (hazimo kwenye picha) mbele ya maafisa aliongozana nao kushiriki uteketezaji wa zana hizo.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (Katikati Mwenye suti ya ugoro) akiwasha moto tayari kwaajili ya kuzitekezeteza zana haramu, kulia ni Juma Makongoro Afisa Mfawidhi Idara ya Uvuvi kanda ya Rukwa na kushoto ni diwani wa kata ya Kirando Kessy Sood.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen kwa pamoja na Mfawidhi Idara ya Uvuvi kanda ya Rukwa Juma makongoro pamoja na Diwani wa Kata ya Kirando Mh. Kessy Sood wakiteketeza zana haramu.
Nyavu zenye thamani ya shilingi milioni 57.6 zikiteketea kwa moto mbele ya wananchi, katika mwalo wa kijiji cha kirando, Ziwa Tanganyika, Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameionya idara ya uvuvi iliyo chini ya wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini kuhakikisha wanawachukulia hatua wale wote wanaokamatwa na zana haramu za uvuvi na kutangaza hukumu zao na si kuishia kwenye kuchoma zana zao tu.

Ameyasema hayo wakati akijiandaa kushiriki zoezi la kuteketeza zana haramu zilizokamatwa kupitia doria katika vijiji vya Kabwe, Isaba, Chongokatete, mandakerenge, kolwe, lupata na kisenga katika wilaya ya Nkasi Mkoani humo. zoezi lililofanyika katika mwalo wa kijiji cha Kirando. 

“Kukamata na kuchoma haitoshi, kwasababu hii inaungua tu, nataka tuwachome wahalifu kwa kutumia sheria, nimechoma sana nyavu hizi na huu mtindo bado unaendelea, hii haina tija, kila tukichoma madhara yanatokea, mazingira yanaharibika, sasa tuseme basi, ningependa kusikia mhalifu kakamatwa kapelekwa mahakamani na kupewa adhabu,” Amesema

Katika kuhakikisha wahalifu hao wanapatika Mh. Zelote amewaasa watumishi wa idara hiyo kuachana na kupokea rushwa, jambo ambalo linaonekana kukwamisha juhudi za serikali katika kulinda rasilimali zake kwaajili ya faida ya kizazi hiki na kijacho.

Amesisitiza kuwa wananchi bado wanahitaji kuendelea kupatiwa elimu juu ya umuhimu wa rasilimali hizo na wajulishwe kuwa rasilimali hizo ni za watanzania wote na hatimae kuacha tabia kuvua samaki hao kwa zana zisizokubalika na sheria za serikali.

Mh. Zelote aliishauri idara hiyo kuwa panapokuwa na zoezi hilo linalofanyika mbele ya wananchi wahakikishe kunakuwa na nyavu halali zinazokidhi viwango vya serikali na kuwaelimisha wananchi tofauti iliyopo ili wasiojua nao wapate kufahamu matakwa ya serikali katika kuhifadhi mazingira.

Kutokana na doria hiyo iliyofanywa na kikosi cha usimamizi wa rasilimali za uvuvi Kijiji cha Kipili kwa kushirikiana na polisi pakmoja na kikosi cha jeshi la wanamaji wote wa kipili kuanzia Juni hadi September 2017 waliweza kukamatanyavu zisizokidhi viwango vya serikali zenye thamani ya shilingi milioni 57.6.

Miongoni mwa nyavu zilizokamatwa ni nyavu 32 za Makira (gilinets) zenye thamani ya shilingi milioni 38.4, nyavu za dagaa zenye macho chini ya 8mm zenye thamani ya shilingi milioni 16.5 na makokoro ya vyandarua yenye thamani ya shilingi milioni 2.7.

Awali akisoma taarifa hiyo fupi ya uteketezaji wa zana haramu za uvuvi kwa mgeni rasmi Afisa mfawidhi idara ya uvuvi kanda ya Rukwa Juma Makongoro alitaja kuwa kuna manufaa mengi yanayopatikana kutokana na rasilimali hiyo ikiwa ni pamoja na watu kujipatia ajira, kitoweo, fedha za kigeni na kuingizia serikali kodi ambayo hutumika kutekeleza miradi ya maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad