HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 6, 2017

NMB yazinduwa matawi saba kwa mpigo katika mikoa sita.

 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya – Amos Makalla (katikakati) akikata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa tawi jipya la NMB Uyole lililopo Jijini Mbeya. Ufunguzi wa tawi hili unafanya idadi ya matawi ya NMB 31 kwa mikoa ya kanda ya Nyanda za juu yaani Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe na Katavi.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya – Amos Makalla akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi la NMB Uyole uliofanyika jijini Mbeya. Ufunguzi wa tawi hili unafanya idadi ya matawi ya NMB 31 kwa mikoa ya kanda ya Nyanda za juu yaani Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe na Katavi.
 Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa Ndani – Augustino Mbogella akizungumza na wateja wa NMB waliokusanyika kushuhudia uzinduzi wa tawi la NMB Mkwajuni wilayani Songwe katika mkoa wa Songwe. Ufunguzi wa tawi hili unafanya idadi ya matawi ya NMB 31 kwa mikoa ya kanda ya Nyanda za juu yaani Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe na Katavi.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Songwe na Mkuu wa Wilaya ya Songwe - Samwel Jeremiah akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Mkwajuni wilayani Songwe, wengine katika picha (kutoka kushoto) Meneja wa NMB kanda ya Nyanda za Juu - Badru Iddy, Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa ndani wa NMB - Augustino Mbogella, Mbunge wa Jimbo la Songwe - Philipo Mulugo, Katibu Tawala wa wilaya ya Songwe - Johari Samizi na Meneja wa Benki NMB Tawi la Mkwajuni - Michael Mzinga. Ufunguzi wa tawi hili unafanya idadi ya matawi ya NMB 31 kwa mikoa ya kanda ya Nyanda za juu yaani Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe na Katavi.

BENKI ya NMB Imefungua matawi saba kwa mpigo katika mikoa sita ikiwa ni juhudi za kujiimarisha zaidi na kuwa karibu na Wateja wake wa kanda ya nyanda za juu.

Matawi hayo yamefunguliwa katika mikoa ya Njombe, Mbeya,Songwe, Rukwa na Katavi. Matawi ambayo yamefunguliwa na yanatoa huduma kwa jamii ni pamoja na NMB  Kasumulu, NMB Uyole, NMB Mkwajuni, NMB Wanging’ombe, NMB Laela na NMB Kalambo lililopo Mlele.

Idadi hii ya matawi mapya inafanya jumla ya matawi ya NMB 31 katika kanda ya Nyanda za Juu huku yakifikia matawi ya NMB 207 nchi nzima.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Tawi la NMB Uyole lililopo mkoani Mbeya, Meneja wa Kanda ya Nyanda za juu - Badru Iddy amesema kuwa lengo la Benki hiyo ni kusogeza huduma zaidi kwa wananchi ili kuwa karibu na wateja wake.

“Kuzinduliwa  kwa tawi hili la NMB Uyole mahali hapa kunafuatia mahitaji ya muda mrefu ya wateja wetu wa Uyole kupata tawi la NMB lenye nafasi ya kutosha .Aidha  eneo hili ni karibu zaidi na wafanyabiashara wengi ambao ni wateja wetu wakubwa na wananchi kwa ujumla. Tawi hili  kama yalivyo matawi yetu mengine nchini linatoa huduma zote za kibenki zitolewazo na benki yetu," alisema Badru.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi la Uyole, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya - Amos Makalla alisema kuwa Wananchi wanapaswa kufungua akaunti katika Benki hiyo na kuitumia kwa kuwa serikali ina hisa ya asilimia 32 katika Benki hiyo.

“Hapa tuelewane, Serikali na Benki ya NMB ni sawa na mapacha kwa kuwa kila mahala ambapo serikali imepeleka huduma zake za kijamii Benki hiyo hufuatia kwa kuweka huduma za kifedha ili kuwahudumia wananchi wa eneo husika,” alisema Mheshiwa Makalla.

Huko Mkoani Songwe Mkuu wa Wilaya ya Songwe  - Samwel Jeremiah ambaye alimwakilisha mkuu wa Mkoa huo  - Chiku Galawa kwenye uzinduzi wa tawi la NMB Mkwajuni, aliwataka wananchi kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha na hivyo kutumia fursa zinazotokana na benki ya NMB kukuza uchumi wao na mwisho kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa kwa ujumla. Alisema desturi ya kuhifadhi fedha  Benki kunajenga nidhamu ya matumizi ya fedha kuepuka madhara ambayo yanaweza kutokea.

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi wa Benki ya NMB Tawi la Mkwajuni, Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa Ndani – Augustino Mbogella alisema kuwa mkakati wa kibiashara wa NMB ni kuhakikisha watanzania wengi zaidi wanapata huduma za kifedha na ndio maana kila wilaya benki hiyo inafungua matawi ili kusogeza zaidi huduma kwa wanannchi.

Alisema kuwa NMB ni benki ya wananchi na wanatakiwa kuitumia kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla kwa kupata huduma zote za kibenki ikiwemo mikopo ya kibiashara katika ngazi mbalimbali.

“Benki ya NMB imeendelea kuwa benki yenye mtandao mpana wa matawi na ATM kuliko benki nyingine yoyote hapa nchini kwa kuwa na matawi zaidi ya 200 huku ikiwa na mashine za kutolea fedha (ATM machines) zaidi ya 700 nchi nzima na Wateja zaidi ya Milioni 2 na laki 5.

Mbogella aliongeza pia kuwa “Benki yetu pia inatoa huduma zote zinazotakiwa kutolewa na benki yeyote ya biashara nchini, tuna akaunti mbali mbali za akiba, huduma za mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya mahitaji yote kwenye soko, huduma za fedha za kigeni, kukusanya mapato na kulipa kwa niaba ya serikali na taasisi mbalimbali”.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad