HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 6 September 2017

BEN POL KUACHIA ALBAMU YAKE YA "THE BEST OF BEN POL' KESHO KUTWA


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Benard Paul 'Ben Pol ' maarufu kama kidume ameamua kuachia albamu yenye nyimbo 15, iitwayo The Best Ben Pol' itakayoanza kuwa mtaani keshokutwa ikiwa ni siku yake maalum ya kuzaliwa.

Mkali huyo wa R n B kesho kutwa Septemba 8 atasheherekea siku yake ya kuzaliwa huku akiachia albamu hiyo, ambayo itakuwa ikimfikisha miaka 8 toka kuanza kwake muziki wa kizazi kipya hapa nchini. 

Akizungumzia ujio wa albamu hiyo pamoja na wimbo wake mpya unaoitwa 'Kidume' ambao 
amemshirikisha mwanamuziki maarufu wa kike kutoka nchini Nigeria Chidinma, alisema kuwa uamuzi wake wa kutoa albamu ni kutaka kuendelea kuwa karibu na mashabiki wake ambao bila ya wao asingefika hapo alipo. 

Ben Pol alisema albamu mpya itatolewa rasmi kesho kutwa ambayo ni siku yake ya kuzaliwa na itakuwa na nyimbo 15, ikiwa na mchanganyiko wa nyimbo mbalimbali ambazo amezifanya kwa kushirikiana na 
wasanii wenzake wa muziki huo. 

"Mimi kama msanii nguli hapa nchini na Afrika Mashariki niliyefanya kazi yangu kwa miaka minane sasa, naona si vibaya kuendeleza muziki wangu kwa kutoa zawadi kwa mashabiki wangu kwa kutoa albamu yangu ya “Best of Ben Pol” ikiwa na nyimbo 15 nilizoshikirisha wasanii mbalimbali wkiwemo Darasa na Rama Dee” alisema Ben Pol. 

Alisema ameamua kufanya hivyo kwa sababu sasa ni mwaka wake wa nane katika safari yake ya muziki ikiwa ni pamoja na kuungana na mashabiki wake ambao wamekuwa wakimuunga mkono kila anapotoa nyimbo zake mpya. 

Albamu hiyo yenye mchanganyiko wa nyimbo mbalimbali ambazo amezifanya na kuweza kufanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya hapa nchini,
ikiwa na nyimbo ijulikanayo kama Kidume, Tatu na Tuliza Boli, ambazo amewashirikisha Darasa na Rama Dee.

Katika kuhakikisha mashabiki wake wanapata vitu vizuri Ben Pol amehakikisha anafanya kazi nzuri katika nyimbo zake hizo mpya kama zile zilizopita ambazo mpaka leo zinaendelea kufanya vizuri na b
aadhi zikiwa Nikikupata, Maneno,Jikubali, Yatakwisha, Sophia, Moyo Mashine, Pete na Phone na 
kama msanii mwenye uwezo katika ukanda wa Afrika Mashariki anaamini kila mshabiki atapenda kupata albamu yake. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad