HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 29 September 2017

  Mshitakiwa James Rugemarila akitoka mahakamani mara baada ya kusomewa mastaka yanayomkabiri. 
Mshtakiwa  Harbinder Singh Sethi (mbele)akitoka katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabiri na mahakama kuamuru kuwa akatibiwe katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ndani ya siku 14 .
Washtakiwa Harbinder Singh Sethi (Mbele) na James Rugemarila wakitoka mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada yamahaka hiyo kuamuru Seth akatibiwe katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ndani ya siku 14 na Kesi hiyo itatajwa tena Oktoba 13, 2017.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru kwa mara nyingine tena  mshtakiwa  Harbinder Singh Sethi akatibiwe katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ndani ya siku 14 ikishindikana Mkuu wa gereza la keko ambako mshtakiwa ndiko anapatikana afike mahakamani kujieleza.

Amri hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi mkuu, Huruma Shahidi wakati kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kusisitiza kuwa amri za mahakama lazima zifuatwe.

Hatua hiyo imekuja baada Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi kudai kuwa kesi imekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika

Baada ya taarifa hiyo, wakili wa utetezi wa Sethi, Joseph Makandege ameieleza mahakama kuwa “licha ya kuwepo kwa amri mfululizo zilizotolewa na mahakama juu ya kutibiwa kwa mshtakiwa Seth katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, mpaka leo  asubuhi tumewasiliana na Sethina ametueleza kuwa, hajapelekwa Muhimbili.

Amedai , kitendo hicho cha kutokutekelezwa kwa amri za mahakama ni ukaidi na kuiomba mahakama itoe adhabu inayostahili kwani wanasigina sheria na kukiuka mamlaka aliyopewa DPP kwani yeye ndio anatakiwa kuongozwa na haja ya kutenda Haki kwani lengo ni kutogeuza mashtaka ya jinai na mahakama kwa nini vyombo vya utesaji.

Alidai kuwa, mashtaka yaliyopo ni mashtaka ya hila ambayo yana lengo la kuupa upande wa mashtaka fursa ya kuwaadhibu washtakiwa hasa mshtakiwa wa kwanza Sethi kabla hawajahukumiwa.

Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Taasisi ya Kumzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),Leonard Swai amedai magereza wamekuwa wakiwatibu wafungwa na mahabusu hata pasipokuwa  na amri ya Mahakama, magereza wapo katika hatua za mwisho, kukamilisha utaratibu wa kumpeleka Sethi Muhimbili.

Kesi hiyo itatajwa tena Oktoba 13, mwaka huu(2017)
Katika kesi hiyo, Sethi na James Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka  mbali mbali ya uhujumu uchumi na utakatishaji USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad