HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 29 September 2017

MADIWANI WA MANISPAA YA SHINYANGA WAPITISHA TAARIFA ZA LAAC NA HESABU ZA MWISHO WA MWAKA 2016/2017

Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Mheshimiwa Agnes Machiya akifungua kikao maalum cha baraza la madiwani leo Ijumaa Septemba 29,2017.-Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog.

Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga limepitisha taarifa miradi zilizotekelezwa katika manispaa hiyo kwa mwaka wa 2016/2017 na taarifa za hesabu za mwisho za halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha ulioishia June 30,2017.
Taarifa hizo zimepitishwa katika kiako maalum cha baraza la madiwani kililofanyika leo Ijumaa Septemba 29,2017 katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna mjini Shinyanga.
Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga,Magedi Magenzi alisema baada ya madiwani kupitisha taarifa hizo zitapelekwa kwa mkaguzi mkuu na mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) na kamati za Bunge Hesabu za serikali za Mitaa (LAAC).
Naibu Meya wa Manispaa hiyo,Agnes Machiya aliwaomba madiwani kuendelea kushirikiano na kushikamana ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Hata hivyo kabla ya taarifa hizo kupitishwa baadhi ya madiwani waliutaka uongozi wa manispaa ya Shinyanga kuacha utaratibu wa kupeleka taarifa zinazohusu masuala ya fedha kwa dharura kwani huenda kuna mapungufu yanaweza kujitokeza matokeo yake madiwani kuonekana wamepitisha taarifa zisizo sahihi.
"Hizi taarifa nyeti za mwisho wa mwaka,zimekuja ghafla tu,kablasha kubwa kama hili ni vigumu kulipitia mara moja,binafsi baada ya kujaribu kulipitia nimebaini kuwepo na mashaka katika baadhi ya miradi,kunaubadhirifu wa fedha",alieleza Diwani wa kata ya Ndembezi David Nkulila.
"Mwaka jana pia mlileta taarifa nyeti kama hizi kwa dharura,Huu uwe mwanzo na mwisho kuleta taarifa kama hizi kwa dharura",aliongeza diwani wa kata ya Kambarage Hassan Mwendapole.
Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga,Magedi Magenzi alisema taarifa hizo zimeletwa kwa dharura kutokana na taarifa hizo kuhitajika mahali panapohusika.
Naibu Meya wa Manispaa hiyo,Agnes Machiya akizungumza wakati wa baraza la madiwani wa manispaa ya Shinyanga leo 
Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga,Magedi Magenzi akizungumza katika kikao maalum cha baraza la madiwani wa manispaa hiyo.
Mchumi wa manispaa ya Shinyanga,Raymond Kilindo akiwasilisha taarifa ya miradi ilizotekelezwa katika manispaa hiyo kwa mwaka wa 2016/2017 na taarifa za hesabu za mwisho za halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha ulioishia June 30,2017.
Diwani wa kata ya Lubaga,Mchungaji Obeid Jilala akiwa katika kikao hicho.
Madiwani wakiwa ukumbini.
Madiwani wakiwa katika kikao hicho.
Diwani wa kata ya Ndembezi David Nkulila akielezea uwalakini wake katika taarifa zilizowasilishwa kwenye kikao hicho.
Diwani wa kata ya Kambarage,Hassan Mwendapole akichangia hoja ukumbini huku akiitaka manispaa ya Shinyanga kuacha kuwa inaleta kwa dharura taarifa zinazohusu masuala ya fedha.
Kikao kinaendelea.
Diwani wa kata ya Mwawaza,Juma Nkwambi akichangia hoja katika kikao hicho. 
Kikao kinaendelea.
Madiwani wakiwa ukumbini.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad