HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 26 September 2017

MBEYA CITY WAMPA KOCHA MRUNDI MKATABA WA MWAkA MMOJA

Kocha Nsanzurwino Ramadhani aliyebeba mikoba ya Kocha Kinnah Phiri kuinoa Mbeya City.Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

KLABU ya Mbeya City imefikia makubaliano na Kocha Nsanzurwimo Ramadhani kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo kwa mkataba wa awali wa Msimu mmoja wa ligi kuu ya Vodacom inayoendelea.

Kocha Ramadhan ni raia wa Burundi na anatarajia kujiunga na timu huko kanda ya ziwa inakoendelea na michezo ya ligi kuu.

Kocha Ramadhani amewahi kuwa kocha kwa nyakati tofauti katika klabu mbalimbali nchini Burundi, Rwanda, Botswana, Malawi, Uganda, na Afrika ya Kusini.

Pia Ramadhan amewahi kuwa mshauri wa ufundi katika timu ya taifa ya Burundi na kocha msaidizi/kocha mkuu wa Muda(caretaker) kwa timu ya taifa ya Malawi.

Mbeya City iliachana na kocha wake Kinnah Phiri takribani wiki mbili zilizopita baada ya kushindwa kutokea kuanzia maandalizi ya msimu mpya mpaka ligi ilipoanza bila kutoa taarifa yoyote kwa uongozi wa timu hiyo.

Kwa sasa Mbeya City wana alama sita wakiwa wameshinda michez miwili na lupoteza miwili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad