HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 26, 2017

JIJI LA MWANZA KUBADILI MFUMO WA ARDHI KUTOKA ANALOJIA KUWA DIGITALI

Na Agness Francis, Blogu ya jamii
 Serikali ya Tanzania wakishirikiana na serikali ya Korea Kusini  wamezindua utekeleza mradi utakaosaidia kuboresha  upatiikanaji wa  huduma bora  za ardhi  katika mkoa  wa Mwanza  na mradi huo  utanzia Manispaa ya Ilemela na Nyamagana.
Ambapo  hafla hiyo ya mradi huo umezinduliwa leo na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Dkt Angeline Mabula  katika ukumbi wa  Hyatt Regency hoteli Jijini  Dar es Salaam.   
Katika ushirikiano huo wa kuimarisha utawala wa ardhi nchini ambapo makubaliano rasmi  ya ushirikiano huo yalianza mwaka 2015, ikiwa ni msada wa vifaa vya upimaji na mafunzo yanayohusu  matumizi ya vifaa vya kisasa vya upimaji, nayo yalianza mwaka 2016.
Naibu waziri Angeline Mabula ametamabaisha kuwa kuleta teknolojia hiyo mpya na nafuu  itarahisishia serikali  upimaji ardhi kwa kupanga na kupima kila kipande, pamoja na kusaidia wananchi kupata kumbukumbu na taarifa za ardhi kwa urahisi.
Mbali na hayo Dkt Angeline Mabula  ametoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Korea Kusini kwa kuona umuhimu wa utekelezaji wa mradi  huo ambao utaleta mapinduzi makubwa  katika sekta ya ardhi hapa nchini.
 Balozi wa Korea Kusini Tanzania, Song Geum-Young  akizungumza na mkurugenzi halmashauri ya Manispaa Ilemela pamoja na wakuu wa idara na taasisi wizara ya ardhi kuhusu ushirikiano uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na Korea Kusini kuimarisha mfumo bora wa upimaji ardhi kwa urahisi.leo katika uzinduzi uliofanyika kwenye ukumbi Hayyat Regency Hotel Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa biashara  wa Kampuni ya LX, Cho Man-Seung akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu kuwa mradi huo unatarajia kuanza kutekeleza  hivi karibuni na  utakuwa ni wa kisasa zaidi hapa Nchini.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Dkt Angeline Mabula akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa maradi wa uboreshaji wa huduma za ardhi leo  uliofanyika kwenye ukumbi wa Hayyat Regency Hotel Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na wakuu wa idara na taasisi wizara ya ardhi waliohudhuria uzinduzi huo leo katika ukumbi Hayyat Regency Hotel Jijini Dar es Salaam. (Picha na Agness Francis, Blogu ya Jamii)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad