HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 4 September 2017

MASHINDANO YA CBA KOMBE LA MWENYEKITI YAFANA

Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa benki ya CBA, Salomon Kawiche (kulia ) akisisitiza jambo  kwa  baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa michuano  ya Mashindano ya Kombe la CBA Golf Mwenyekiti  yaliyothaminiwa na benki hiyo ,yaliyofanyika kwenye viwanja vya Lugalo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa benki ya CBA,Dkt. Gift Shoko (katikati)akiongea na wa chezaji wenzake wa Golf  Dkt. Edmond Mndolwa (Kushoto) na Joseph Marwa (kulia)wakati wa michuano  ya Mashindano ya CBA Golf ya Kombe la Mwenyekiti  yaliyodhaminiwa na benki hiyo,yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Lugalo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CBA ,Dkt. Gift Shoko, akipiga mpira wa golf wakati wa mashindano ya CBA  Kombe la Mwenyekiti yaliyodhaminiwa na benki hiyo ,yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya golf vya Lugalo jijini Dar es Salaam.
 Mshindi wa jumla wa  mashindano ya CBA   Kombe la Mwenyekiti, Samson Mwingi,akikabidhiwa zawadi ya TV na  Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa benki ya CBA ,Dkt.Gift Shoko,Baada ya mashindano hayo kuisha yaliyofanyika kwenye viwanja vya golf vya Lugalo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya golf ya Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo.
  Iadan Nzuki  ambaye aliyeibuka mshindi wa kwanza wa divission A wakati wa mashindano ya  Golf ya kuwania CBA   Kombe la Mwenyekiti,akipokea zawadi ya saa toka kwa Mkuu wa kitengo cha rasmali watu (HR) wa benki ya CBA ,Zainabu Mushi(kushoto) mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya golf vya Lugalo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa benki ya CBA ,Dkt.Gift Shoko(wapilia kushoto)  pamoja na baadhi ya viongozi wa Golf  klabu ya Lugalo  wakimshuhudia mwanamuziki mkongwe wa bendi ya Mark band, Rashidi Pembe akionyesha umahiri wake kwenye hafla ya kuwapongeza washiriki wa  mashindano ya CBA   Kombe la Mwenyekiti,yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya golf vya Lugalo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad