HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 19 September 2017

MARUBANI WAZAWA WANAHITAJIKA KATIKA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA KWA MAENDELEO YA NCHI-PROFESA MBARAWA.

Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa akiongea na Balozi wa Ufaransa nchini, Bi. Malika Berak mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere katika Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Usafiri wa Anga lililoanza leo.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (mwenye tai nyekundu waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Kwanza la Usafiri wa Anga linalofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Kushoto kwa Waziri  ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi na kulia Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Bw. Hamza Johari. 
.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SERIKALI imesema kuwa inatatizo la mabaruni wa kurusha ndege hali ambayo inahitaji kusomesha marubani kwa wingi na kuacha kuchukua nje ya nchi.

Hayo ameyasema Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa sekta ya usafiri wa Anga leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mbarawa amesema kuwa sasa ni wakati wa kusomesha marubani, mafundi pamoja wahandisi wa ndege kutokana na mahitaji ya hao wote katika kufikia uchumi wa kati wa 2025.

Amesema kuwa hakuna sababu ya watu hao kuchukua nje ya nchi wakati malengo ya serikali kwenda kwa kasi katika maendeleo ya sekta ya usafiri wa anga ambayo ndiyo itafanya kuongeza kwa pato la taifa pamoja na uchumi.

Mbarawa amesema kuwa serikali imejipanga katika ujenzi wa miundombinu ikiwemo miundombinu ya viwanja vya ndege katika na kuweza kufanya Tanzania kuwa kiunganishi kwa safari za ndege za nchi mbalimbali.
Aidha amesema kuwa wanahitajika wawekezaji makini katika sekta ya usafiri wa anga na sio wawekezaji wa kufanya blablaa na kufanya sekta hiyo ishindwe kukua kwa kasi katika malengo ya serikali.

 Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema kuwa mkutano huo utajadili mada mbalimbali ikiwemo kupungua kwa shehena katika viwanja vya ndege pamoja na bidhaa zinazozalishwa nchini kutumia viwanja nchi jirani ambapo wadau ndio wenye majibu ya kuweza kuitatua changamoto hiyo.

Johari amesema kuwa katika  mkutano huo ni muhimu katika sekta ya usafiri anga  katika kuboresha huduma ili iweze kwenda kwa kasi katika ukuaji wa uchumi.


Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege Nchini (ATCL), Ladislaus Matinde amesema mahitaji ya ndege duniani 39620 kwa Afrika ni 10150  huku marubani 617000  duniani na Afrika 22000 na Mafundi 814000, Afrika Mafundi wa Ndege 24000.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad