HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 11, 2017

MAHAKAMA YA YATOA SIKU SABA KWA UPANDE WA MSHTAKA juu ya hatma ya upelelezi

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetoa siku saba kwa upande wa mashtaka watoe msimamo wao juu ya hatma ya upelelezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili waliokuwa mabosi wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (RAHCO), wanaokabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababisha serikali hasara ya dola 527, 540 za Marekani.

Hakimu Thomas Simba ameyasema hayo mapema leo, kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa na upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa serikali, Patrick Mwita ulidai kuwa upeleelezi haujakamilina nab ado wanaendelea kuandaa taarifa ili kupeleka kesi hiyo Mahakama Kuu ili ianze kusikilizwa.

Hata hivyo Hakimu Simba alitaka kufahamu taarifa hiyo inayoandaliwa itachukua muda gani, Mwita amedai kutokana na unyeti wa kesi yenyewe ndio maana linachukua muda mrefu.

Mshtakiwa Kanji alinyoosha mkono kuiomba mahakama kuingilia kati suala hilo ili  lifikie mwisho na wapate kujua hatma yao kwani upande wa mashtaka hauna sababu za msingi za kuendelea kuwashikilia na kwamba wanaona haki zao zinakiukwa.

Hakimu Simba amewapa upande wa mashtaka siku saba kukamilisha suala hilo na kuwaeleza kuwa huo ni ujumbe makini sana.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Mhandisi Benhard Tito, Raia wa Kenya anayedaiwa kuwa dalali wa zabuni, Kanji Mwinyijuma na aliyekuwa Katibu wa kampuni hiyo, Emmanuel Massawe. Kesi hiyo itakuja tena Septemba 18 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad