HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 20 September 2017

LIGI NDOGO YA WANWAKE YAPELEKWA MPAKA SEPTEMBA 30

Mwenyekiti wa Chama cha Soka Wanawake (TWFA) Amina Karuma.Ligi Ndogo ya Wanawake sasa itaanza rasmi Septemba 30, 2017 katika Kituo cha Dar es Salaam badala ya Septemba 22, mwaka huu.

Wakati tayari timu zimepewa taarifa rasmi juu ya tarehe hiyo mpya, lakini kwa taarifa hii, timu zilizoko mikoani zisianze safari kwa sasa.

Kupelekwa mbele kwa tarahe husika kumetokana na taratibu za mwisho za usajili ambako sasa timu bingwa wa mkoa inayotambuliwa na mkoa, lazima itimize masharti matatu.

Kwanza; Ni kuthibitisha kushiriki kucheza ligi ndogo kabla ya Septemba 25, mwaka huu.

Pili; kuthibitisha kama imesajiliwa kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo (Klabu iwe na hati ya usajili) na tatu kuwasilisha majina ya wachezaji wake iliyowasajili kwa .

Kama kuna timu bingwa kwa mujibu wa mkoa, na tayari ina majina ya wachezaji iliyowasajili msimu huu, lakini haina hati ya usajili kutoka kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya mchezo, basi klabu hiyo itakosa sifa ya kushiriki.

Sharti kubwa ni kwamba timu au klabu hiyo lazima iwe imesajiliwa kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo. Ndio utaratibu.


Ligi Ndogo inachezwa ili kupata timu mbili zitakazopanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara msimu wa 2017/18 baada ya timu mbili kushuka msimu wa 2016/17.

Ligi ya msimu ulipita bingwa ni Mlandizi Queens ya Pwani wakati zilizoshuka daraja ni Viva Queens ya Mtwara na Victoria Queens ya Kagera.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad