HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 16 September 2017

KAMPUNI MPYA YA USAMBAZAJI WA KAZI ZA WASANII YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR

 Jengo la Kampuni mpya ya usambazaji wa kazi za wasanii wa Bongo Movie, lililopo Kinondoni Hananasifu, Jijini Dar es salaam. Uongozi wa Kampuni hiyo umefanya Uzinduzi wake rasmi jioni hii na kuhudhuliwa na Wasanii mbalimbali pamoja na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kampuni ya Treeo Tabasamu, John Kallaghe akifafanua jambo wakati wa Mkutano na waandishi wa habari katika uzinduzi rasmi wa Kampuni hiyo, uliofanyika jioni hii katika ofisi zao, Kinondoni Hananasifu, Jijini Dar es salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Ritchie Mtambalike pamoja na Mkuu wa Kitengo za Masoko wa Kampuni ya Treeo Tabasamu, Jacob Steven (JB).

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Treeo Tabasamu, Ritchie Mtambalike akizungumza katika Uzinduzi rasmi wa Kampuni hiyo, jioni hii katika ofisi zao, Kinondoni Hananasifu, Jijini Dar es salaam.  
Mkuu wa Kitengo za Masoko wa Kampuni ya Treeo Tabasamu, Jacob Steven (JB) akizungumza katika Uzinduzi rasmi wa Kampuni hiyo, jioni hii katika ofisi zao, Kinondoni Hananasifu, Jijini Dar es salaam. 
Jaqueline Wolper ni mmoja wa wasanii waliohudhulia uzinduzi huo.
Ankal Issa Michuzi (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na JB, Ritchie pamoja na Dude.
Ankal na vijana wake.
Muonekani wa Jengo hilo kwa mbele.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad