HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 1 September 2017

ILIYOTUFIKIA: MAHAKAMA KUU KENYA YAAMURU UCHAGUZI URUDIWE NDANI YA SIKU 60

MAHAKAMA Kuu nchini Kenya (Supreme Court), imebatilisha ushindi wa uRais wa Rais wa sasa Uhuru Kenyatta, dhidi ya mpinzani wake mkuu Raira Odinga, na kuamuru uchaguzi huo urudiwe ndani ya siku 60 kuanzia leo Septemba 1, 2017. 

Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo, kufuatia maombi ya Mgombea Urais wa Muungano wa upinzani wa NASA, Raila Odinga baada ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais, uliompa ushindi Rais Kenyatta. 

Katika maombi yake,  Odinga alisema, kura zake zilipunguzwa kwenye baadhi ya vituo na kuongezewa mpinzani wake, lakini kubwa zaidi ni kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi ambapo baadhi ya fomu muhimu za matokeo ya uchaguzi kama vile fomu namba 34A,B na C, hazikupatikana siku ya kutangazwa kwa matoko. 

Katika uamuzi wa mahakama hiyo, majaji wanne kati ya sita (6), wamekubaliana kuwa tume huru ya uchaguzi na mipaka ya Kenya, (IEBC), imeshindwa kusimamia vema uchaguzi huo na hivyo kusababisha kasoro kadhaa ambazo zinakwenda kinyume na katiba ya Kenya. Hata hivyo, Mahakama hiyo imesema, hakuna ushahidi wowote, ulioonyesha kuwa Rais Uhuru Kenyatta, alitenda makosa katika mchakato huo wa uchaguzi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad