HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 26 September 2017

DC ATEMBEZA BAKULI KWAAJILI YA UJENZI WA ZAHANATI.

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuja Juma Homera kushoto akipokea Cheki ya Shilingi Milioni moja kutoka kwa mkurugezi wa kampuni ya kuuza mafuta ya OIL COM mjini hapa kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Nakayaya mjini hapa. Na Steven Augustino wa Ruvuma TV Tunduru SERIIKALI imewataka wadau mbalimbali wa maendeleo kujitokeza kusaidia ujenzi wa Kituo cha Afya cha Afya Nakayaya Mjini hapa na Kwamba baada ya kukamirika kwa ujenzi huo kituo hicho kitasaidia kupunguza msongamano katika Hospitali ya Serikali ya wilaya ya Tunduru.

 Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma Juma Homera wakati akipokea msaada wa Shilingi Milioni 1,400,000 kutoka kwa mkurugenzi wa Kituo cha kuuza mafuta cha OIL COM Mjini hapa na kutolewa kwa kwamba msaada huo kutasaidia kukamirika kwa baadhi ya shughuli za ujenzi huo.Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera akionyesha Zahanati ya Kata ya Nakayaya ambayo inaendelea kujengwa. Aidha katika taarifa hiyo pia dc Homera ametumia nafasi hiyo kuwapongeza baadhi ya wadau wa maendeleo wa ndani la nje ya wilaya hiyo kwa kujitokeza na kumuunga mkono juhudi za Serikali katika ujenzi wa Kituo hicho kwa lengo la kuwasogezea huduma wananchi. 

Alisema pamoja na michango hiyo kutoka kwa wadau pia serikali inatengeneza utaratibu wa kuwashirikisha wananchi katika ujenzi huo ili nguvu kazi watakayo itoa iweze kusaidia kupunguza gharamaa za ujenzi. Tayali ujenzi Zahanati hiyo umekwisha anza na kukamilisha jengo la Utawala katika kituo hicho na kwamba hadi kukamilika kwa ujenzi wa majengo yote 8 yaliyopangwa kughalimu zaidi ya shilingi 419. 

 Akizungumzia tukio hilo Mkurugenzi wa Kituo cha mafuta Cha OIL COM Bw. Ghulam Kalamal alisema kuwa msaada huo ni sehemu ya kampuni yake kurudisha faida iliyopata kutokana na biashara hiyo ili iweze kuhudumia jamii katika eneo hilo. Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Goerge Chiwangu amesema kuwa zaidi ya Wagonjwa wanje 100 hufikana kupatiwa matibabu kwa siku huku kukiwa na kundi la kaati ya akina mama 15 na 20 ambao hufika hospitalini hapo kwa lengo la kijifungua. Hii hapa Video yake .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad