HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 6 September 2017

BUSWITA RUKSA KUCHEZA YANGA, ATAKIWA KUILIPA SIMBA MILIONI 10Kamati ya Sheria katiba na hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF wamemfungulia adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja iliyokua inamkabili mchezaji Pius Buswita ambaye alifungiwa kutokana na kusaini mikataba miwili na timu za Yanga na Simba.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari asubuhi ya leo Mwenyekiti wa kamati hiyo Wakili Elias Mwanjala amesema Simba,Yanga na Mchezaji mwenyewe wamekubaliana Pius Buswita alipe pesa alizochukua katika klabu ya Simba wakati akisaini mkataba wa makubaliano ya kuichezea klabu hiyo.

Wakili Mwanjala amesema kilichofanywa na klabu hizo mbili ni busara tu ili kumpa nafasi mchezaji huyo acheze kinyume cha hapo mchezaji huyo angeendelea kutumikia adhabu yake na walichokitaka Simba wao ni kulipwa tu pesa zao ili kuondoa lalamiko hilo na mchezaji mwenyewe ameahidi mbele ya kamati kwamba atalipa.

Kiasi cha milioni 10 pamoja na gharama zingine ikiwa ni pamoja na usafiri na malazi ambazo kwa pamoja zinafikia milioni 1 ndizo zilizotajwa na Simba kwenye barua yao waliyoiwasilisha TFF na ndicho kiasi ambacho Yanga na mchezaji wameahidi kulipa na kamati imetoa onyo kali la kimaandishi kwa mchezaji huyo na ataruhusiwa kucheza tu iwapo Simba watathibitisha kulipwa pesa zao.

Buswita mchezaji wa zamani wa Mbao FC ya Mwanza alijikuta akifungiwa na shirikisho la soka nchini baada ya kusajiliwa na Yanga huku pia akiwa amesaini mkataba na Simba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad