HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 30 September 2017

BARAZA TAIFA LA TAFES LAZINDUA SIKU 40 ZA MAOMBI KUOMBE AMANI NA WANAFUNZI WATAKAOANZA MASOMO VYUONI.
BARAZA la taifa la TAFES hapa nchini limezindua siku 40 za maombi kwaajili ya kuombe amani hapa nchini pamoja na wanafunzi watakaoanza mwaka mpya wa masomo katika vyuo vikuu vyote hapa nchini.


Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa baraza la taifa la TAFES, Profesa Lazaro Busagala wakati akizungumza na wanafes waliohudhulia mkutano wa chama hicho jijini Dar es Salaam leo.

Nae Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba, amesema kuwa ili kuwa na taifa lenye maadili lazima kuwe na taasisi za kidini na za kiroho zitakazokuwa zikiwalea watoto na vijana katika vyuo hapa nchini, pia amesema kuwa Baraza la taifa la Tafes ambalo linawalea wanafunzi wa vyuo vikuu wa madhehebu ya kiprotestandi yanafanya kazi kubwa sana kwa kuwalea wanafunzi hao wawapo vyuoni na kuwa na maadili yanayokubalika katika jamii.

Amesema kuwa ili kuwa na jamii yenye maadili lazima kuwepo na watu wenye karama ya kuwafunza wengine maadili ya kiroho.
Mtoa maada Dk. Joshua Wathang'a akizungumza kuhusiana na kwanini huduma ya kiroho itolewe vyuoni kwa wanafunzi hii kwasababu elimu hii humwandaa mwanafunzi kukubalika katika jamii pamoja na kuwa na watu wenye hufu ya Mungu na wenye maadili mazuri.Wathang'a ameyasema hayo mbele ya wanachama wa TAFES waliohudulia katika mkutano huo jijini Dar es salaam.
Mnyekiti wa baraza la taifa la TAFES, Profesa Lazaro Busagala akizungumza na wanafes waliohudhulia mkutano wa chama hicho jijini Dar es Salaam Uliofanyika kwaajili ya Kuombea Taifa pamoja na wanafunzi watakaoanza mwaka mpya wa masoko katika vyuo vikuu hapa nchini.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba, akizungumza na wanachama wa Taasisi ya wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini wakati wa kuzindua siku 40 za maombi kuombea Nchi pamoja na wanafunzi watakao jiunga na vyuo vikuu wa dini za kiprostandi hapa nchini.Taasisi hiyo ambayo inasaidia kuwaandaa kiroho na kijamii wanafunzi ili kuwe na jamii adilifu pamoja na viongozi waadilifu.
Taasisi hiyo inamchango mkubwa katika kuitengeneza jamii kuondokana na jamii yenye watu wenye roho mbaya.
 Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Felchesmi Mramba akizungumza na wanaTAFES  walikusanyika katika ukumbi wa mikutano wa benki kuu jijini Dar es salaam.Baadhi ya wageni waliohudhulia katika mkutano wa wanaTAFES wakimsikiliza Mgeni rasmi jijini Dar es Salaam.
  Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Felchesmi Mramba Akiwa katika mkutano wa wanatafes uliofanyika jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuliombea taifa amani pamoja na kuwaombe wanafunzi watakaoanza mwaka mpya wa masomo mwaka huu.Baadhi ya wageni waliohudhulia katika mkutano wa wanaTAFES wakimsikiliza Mgeni rasmi jijini Dar es Salaam. 

Picha zote na Avila Kakingo,Globu ya jamii

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad