HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 6, 2017

Airtel na VETA watoa semina ya mafunzo ya ujuzi kwa Vijana Dar

Meneja Miradi Airtel Tanzania Jane Matinde akizungumza wakati wa semina kwa vijana kuhusu umuhimu wa kusoma kwa kutumia mtandao kupitia aplikesheni ya VISOMO inayotumiwa na VETA kwa kushirikiana na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo Morocco, Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Magilatech Company Ltd. Godfrey Magila na mtaalamu wa tenklojia akitoa mafunzo kwa vijana waliodhuria semina kuhusu umuhimu wa kusoma kwa kutumia mtandao kupitia aplikesheni ya VISOMO inayotumiwa na VETA kwa kushirikiana na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo Morocco, Dar es Salaam jana.
Baadhi ya washiriki wa semina kwa vijana kuhusu umuhimu wa kusoma kwa kutumia mtandao kupitia aplikesheni ya VISOMO inayotumiwa na VETA kwa kushirikiana na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakifuatilia kwa umakini mafunzo yaliokuwa yanatolewa kwa ajili ya kuwahamamisha jana jijini Dar es Salaam.


Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikia na VETA leo wametoa mafunzo kwa vijana mkoani Dar itakayowawezesha kuongeza ujuzi na kuenda sambamba namahitaji ya soka la ajira na kujiajiri.
Mafunzo hayo yenye lengo la kutoa fursa mbalimbali zinazopatikana kupitia ushirika wa watoa huduma hao yanalenga katika kuwawezesha vijana nchnini  kujiendeleza kielimu kupitia application ya VSOMO kwa kupata masomo ya ufundi stadi ya VETA kupitia simu zao za mkononi ili kuongeza ujuzi wao
Akiongea wakati wa semina hiyo , Meneja Mradi wa Airtel, Bi Jane Matinde alisema Tumeonelea vyema kufanya semina hii ili kuongeza uelewa kwa vijana  juu ya fursa hii muhimuinayotoa nafasi ya kijana kujitambua na kujiajiri mwenyewe mara baada ya kusoma masomo ya Ufundi kupitia simu zao za mkononi na kupata cheti.  Tunao vijana Zaidi ya wateja 30,000 ambao wamepakua application ya VSOMO kati yao 9,000 wamejiandikisha ili kusoma kwa mtandao lakini idadi ya waliopata vyeti bado ni chache, hivyo tumeonelea ni vyema kujikita katika kutoa elimu na kuwahamashisha watanzania kutumia technologia hizi za kisasa kujisomea wakati wowote mahali popote kupitia simu zao za smartphone na hatimae kufanya mafunzo ya vitendo na kupata cheti
Tunatoa wito kwa watanzania hususani vijana kuchangamkia fursa hii kwa kupakua application ya VSOMO kwenye simu zao na kusoma kozi hizi za ufundi ambazo gharama yake ni 120,000/= hadi kumaliza na kupata cheti.
Kwa upande wake mtaaalamu wa technologia na Mkurugenzi wa Magilatech Company Ltd. Bw, Godfrey Magila alisema, Techonologia inakuwa kwa kasi sana ni muhimu kutumia Tehama katika kuleta tija katika kibiashara, kilimo , elimu na kadhalika. Kwa kuona hivyo tumeanzisha hii application ya VSOMO ambayo ni ya kwanza dunia kutoa mafunzo ya ufundi kupitia simu na Tanzania tunajivyunia kupiga hiyo muhimu.
Naye Meneja Mradi wa VSOMO VETA , Bwana Charles Mapuli alisema, Ushirikiano wetu na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kunaongeza wito katika kutoa elimu ya ufundi na kuwafikia watanzania wengi Zaidi. Napenda kuwahakikishia kuwa masomo haya ya VETA kupitia simu yamehakikiwa na VETA kuhakikisha yanatolewa katika ubora na viwango vinavyotakiwa, na hivyo natoa wito kwa watanzania kutumia fursa hii kujiendeleza.  Lengo letu ni kuhakikisha kila mtanzania anapata fursa ya kujiendeleza na kuwa na ueledi utakaomuwezesha kuajiriwa au kujiajiri. 
Kozi zinazopatikana katika application ya VSOMO ni pamoja ni  Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo ya kompyuta,umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani, Umeme wa magari. Vilevile Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi wa simu za mkononi, Ufundi Alluminium,  Utaalamu wa maswala ya urembo pamoja ma Ufundi wa kuchomea vyuma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad