HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 30, 2017

Waziri Mbarawa aridhishwana kasi ya ujenzi TBIII

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Prof. Makame Mbarawa (kulia) akisikiliza maelezo ya ujenzi wa mradi wa jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), kutoka kwa Meneja wa mradi, Bw. Ray Blumrida.

Na Neema Harrison, TUDARCO

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Prof. Makame Mbarawa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, ambapo sasa utakamilika Oktoba 2018. Mhe. Prof. Mbarawa aliyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea maendeleo ya mradi huo ulianza 2013, na sasa kuridhishwa na hatua waliyofikia. Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo, Prof. Waziri Prof. Mbarawa amesema kwa sasa ujenzi umefikia asilimia 64, na hatua iliyobaki ni ujenzi wa wa mifumo ya ndani ya jengo.

“Sote tumekuwa mashahidi nimekuwa nuikitembelea mara kwa mara ujenzi wa jengo hili na ninaridhika kwa kasi ya ujenzi wake, ambapo sasa tumefikia kwenye hatua nzuri na vitu vilivyobaki sio vikubwa kama ilivyokuwa wakati wanaanza, hivyo ni matumaini yangu hadi Oktoba mwakani (2018) jengo lote litakuwa limekamilika na serikali kukabidhiwa,” amesema Mhe. Prof. Mbarawa. Hatahivyo, Prof. Mbarawa amesema serikali inatarajia kupata watalii wengi na serikali itapata mapato kupitia kodi na tozo za abiria wanaosafiri kutumia kiwanja hiki, pia wapangaji wanaotoa huduma mbalimbali yakiwemo maduka na usafiri wa magari.

Amesema serikali itaendelea kutoa fedha za ujenzi wa jengo hilo linalosimamiwa na mkandarasi BAM International ya Uholanzi, ambapo pia likikamilika litatoa ajira kwa Watanzania wengi.

“BAM wamekuwa wakifanya kazi nzuri nawapongeza sana na tunatarajia hadi kukamilika tutapata mradi bora utakaoliingizia taifa faida kubwa kutokana na kodi na tozo mbalimbali,” amesema Prof. Mbarawa. Amesema jengo hilo likikamilika linatarajia kuchukua abiria milioni sita (6) kwa mwaka, na kupunguza msongamo ulipo katika jengo la pili la abiria (JNIA-TBII)
Mkurugenzi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Wolfgang Marschick (kushoto) akiwa na Mhe. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akikagua mradi wa jengo hilo.
Mhe. Prof. Makame Mbarawa mwenye miwani mkononi, akiendelea leo na ukaguzi wa ujenzi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Kushoto ni Mkurugenzi wa mradi huo Bw. Wolfgang Marschick na kulia ni Meneja wa Mradi Bw. Ray Blumrida.
Meneja wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Bw. Ray Blumrida (wa pili kulia) akielezea ujenzi wa ngazi zinazotumia umeme (escalator) kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Prof. Makame Mbarawa alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo leo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Prof. Makame Mbarawa (katikati), akimsikiliza Meneja wa mradi wa jenzi la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Ray Blumrida akielezea ujenzi wa madaraja (bridges) ya kupitia abiria wanaowasili na wanaoondoka.
Mhe. Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto), akifurahia jambo na Mkuu wa Kitengo cha Ujenzi wa Viwanja vya Ndege cha Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Emmanuel Raphael wakati wakitoka kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad