HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 29 August 2017

WATU SITA WAFARIKI KWA AJALI YA LORI KIJIJI CHA KATIKA KIJIJI CHA KIJOTA, SINGIDA.

Watu sita wamefariki dunia huku wengine 42 wakijeruhiwa baada ya lori lenye namba za usajili T.806 AEL aina ya scania mali ya Abdalla Mussa (39) mfanyabiashara mkazi wa Mwenge mjini Singida, kuacha njia na kupinduka katika Kijiji cha Kijota, Singida.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba amesema ajali hiyo imetokea Agosti 27 mwaka huu saa 1.30 usiku katika kijiji cha Kijota wakati likitokea mnadani katika kijiji cha Mtinko Singida vijijini, likielekea Singida mjini.

ACP Magiligimba ametaja chanzo cha ajali kuwa ni uzembe wa dereva wa lori hilo Jumanne Kidanka (32) Kamanda huyo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva ambaye hakuwa makini akiwa anaendesha lori hilo lililosheheni abira na mizingo mingi.

Amewataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Haji Jumanne (35), Mikidadi Mohammed (40) wote wawili wakazi wa kijiji cha Mrama na Musa Salimu (30) mkazi wa kijiji cha Mwakiti.

ACP Magiligimba amewataja wengine kuwa ni Allen Mwangu (38) mkazi wa wilaya ya Ikungi, Lucas Stephano (40) mkazi wa kijiji cha Mrama na Sharifa Omari (19) mkazi wa kijiji cha Ilongero.

Ameongeza kuwa majeruhi 20 wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Singida, kumi wamelazwa hospitali ya misheni ya Mtinko na wanne ambao hali zao ni mbaya, wamelazwa katika hospitali ya misheni ya Hydom mkoani Manyara.

Ameeleza kuwa baadhi ya majeruhi walipatiwa matibabu na kurejea makwao huku wengine waliolazwa wamevunjika mikono, miguu na sehemu mbalimbali ya miili yao.

“Hawa wenye hali mbaya ni Fadhili Jumanne (33) mkazi wa Kibaoni mjini Singida, Mikidadi Hamisi, Jafari Hamisi na Idrisa Ibrahimu, wote wamevunjika miguu. Miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye hospitali misheni Mtinko”, amesema.
 Mmoja wa majeruhi akipatiwa matibabu ya mkono katika hospitali ya Mkoa wa Singida mara baada ya kupata ajali ya lori iliyoua watu 6 katika kijiji cha Kijota Singida.
 Mmoja wa majeruhi akiwa amelazwa huku akiendelea kupatiwa matibabu ya mkono katika hospitali ya Mkoa wa Singida mara baada ya kupata ajali ya lori iliyoua watu 6 katika kijiji cha Kijota Singida.
Baadhi ya ndugu na jamaa wa majeruhi wa ajali ya lori iliyoua watu sita wakiwa nje ya wodi za wagonjwa katika hospitali ya Mkoa wa Singida.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad