HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 29 August 2017

MCHUNGAJI KUTOKA NCHINI GHANA KUTOA HUDUMA KWA SIKU TATU KATIKA KANISA LA PURE FIRE MIRACLES LILILOPO TABATA SEGEREA.

MWAZILISHI na mchungaji Mkuu wa kanisa  la Moto halisi (Pure Fire miracles Ministries International'), lililopo Tabata Segerea kwa Bibi
,Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana amewasili hapa kwaajili ya
  kuwaletea siku tatu za huduma ya ujazo wa upako.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha hapa nchini mchungaji huyo kutoka nchini Ghana, Mchungaji Mwenyeji, Innocent Ikechukwu amesema kuwa wananchi wajitokeze ili kupata maada mbalimbali za ukombozi na mafanikio.

Amesema huduma zitatolewa kwa siku tatu kuanzia leo Jumanne saa 11:00 jioni hadi alhamisi ambapo wahapingani kabisa na muda wa kazi hapa nchini kutokana na muda huo watu wengi watakuwa wametoka makazini.

Huduma hiyo itatolewa kwa lengo la kusaidia wanachi wenye matatizo mbalimbali, ili kupata upanyaji na kumtumaini Mungu,pamoja na Ukombozi na Mafanikio ambapo wanawaalika watu mbalimbali kuhudhulia mkutano huo ambapo mtoa maada katika siku tatu mfululizo ili kujipatia huduma za ukombozi na mafanikio.

 Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana akiwapungia mkono waumini wa kanisa la Pure Fire miracles Ministries International jijin Dar es Salaam leo mara baada alipowasili jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mchungaji Mwenyeji, Innocent Ikechukwu.
 Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana akiwasalimia waumini wa Kanisa la Moto halisi jijini Dar es Salaam leo.
 Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana akisalimiwa na muumini wa kanisa la Moto halisi jijini Dar es Salaam leo.
Kikundi cha Mtalumbeta wakitumbuiza katika ujio wa
Mwanzilishi na mchungaji Mkuu wa kanisa  la Moto halisi (Pure Fire miracles Ministries International') mara baada alipowasili hapa nchini jijini Dar es Salaam leo.
 Waumini wakanisa la Pure Fire miracles Ministries International' wakimshangilia na kumkaribisha
Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana mara baada alipowasili kanisani hapo jijini Dar es Salaam leo.
 Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana wakimshangilia mwanzilishi wa kanisa lao mara baada alipowasili jijini Dar es Salaam leo.
 Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana akizungumza na waumini  mara baada alipowasili jijini Dar es Salaam leo kushoto ni Mkalimani.
 Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana akizungumza na waumini wa Kanisa la Moto halisi (Pure Fire miracles Ministries International') lilopo Tabata Segerea kwa Bibi jijini Dar es Salaam mara baada alipo wasiri hapa nchini majira ya saa 6: 30 na kuzungumza machache na waumini wa kanisa hilo kuhusu huduma atakayoitoa kwa waumini hao.
 Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kuwasili katika Kanisa la Moto halisi (Pure Fire miracles Ministries International') lilopo Tabata Segerea kwa Bibi jijini Dar es Salaam.
 Mchungaji Mwenyeji, Innocent Ikechukwuakizungumza wakati wa kumkaribisha  Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana mara baada alipo wasili kanisani hapo jijinio Dar es Salaam leo.
Pia amemshukuru kwa kuitikia wito wake kuja hapa nchini kutoa huduma ya neno la Mungu pamoja na ukombozi wa Mafanikio ya wanajamii watakao hudhuria katika huduma kanisani hapo.
Baadhi ya waumini wa Kanisa la Moto halisi (Pure Fire miracles Ministries International') lilopo Tabata Segerea kwa Bibi wakimuaga Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana mara baada ya kufika na kuongea na waumini hao.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad