HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 22 August 2017

Washindi droo ya weka amana na Benki ya CBA wapatikana

BENKI ya CBA, jana iliendesha droo yake ya kwanza katika kampeni ya kuhamasisha umma kujiwekea  akiba inayojulikana kama ‘weka amana ushinde’ ambapo washindi wawili walipatikana na kujinyakulia kiasi cha shilingi milioni tatu

Jesen Anderson Mbise kutoka Arusha aliibuka mshindi kwa upande wa wateja binafsi na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni moja, huku Hoteli ya Tiffany ya jijini Dar es Salaam wakiibuka washindi katika upande wa taasisi na kujinyakulia shilingi milioni 2.

Zaidi ya shilingi milioni 20 zimetengwa kwa ajili ya kutolewa kama zawadi katika kampeni hiyo ambayo itakayodumu kwa kipindi cha miezi mitatu.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuchezeshwa kwa droo hiyo ambayo ilishuhudiwa na mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha,  Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa CBA Gift Shoko alisema lengo la promosheni hiyo ni kuhamasisha umma kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba.

”Kampeni hii inalenga kuwahamasisha wateja wetu waliopo na watarajiwa kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba. Kuweka akiba ni muhimu kwa kuwa kunawezesha kufanya uwekezaji pamoja na kupambana na matukio yasiyotarajiwa ambayo yanahitaji fedha,” alisema Shoko

Alisema kujiwekea akiba ni muhimu haswa katika kipindi hiki kinachoelekea mwisho wa mwaka ambapo huwa na mahitaji makubwa ya kifedha kwa ajili ya shughuli kama kulipa ada za shuke, kodi za nyuma, likizo pamoja na shughuli nyingine. Kwa mujibu wa Shoko, benki ya CBA imerahisisha namna ya wateja wake kujiwekea akiba ambapo wanaweza kutumia simu zao za kupitia huduma ya M-PAWA, kwa kutumia njia ya mtandao pamoja na kutembelea matawi yake yaliyopo sehemu mbali mbali.

Benki ya CBA kwa sasa ina matawi 11, matano yakiwepo jijini Dar es Salaam huku matano yakiwepo Arusha, Mwanza, Mbeya, Mtwara, Moshi, na Tunduma.
Mkurugenzi wa benki ya CBA, Gift Shoko,( kulia) akibofya kitufe cha kompyuta kuashiria Uzinduzi wa droo ya kwanza ya promosheni ‘Weka amana Ushinde’ zaidi ya milioni 20 zitashindaniwa na wateja wa benki hiyo. Katikati ni Mkuu wa kitengo cha biashara wa benki hiyo,Mussa Kitambi na Msamimamizi wa michezo wa kubahatisha nchini Abdallah Hamedi. 
Mkurugenzi wa benki ya CBA, Gift Shoko, ( watatu kushoto) akimshuhudia Mkuu wa kitengo cha biashara wa benki hiyo, Mussa Kitambi(Kushoto) alipokuw akimpigia simu mkazi wa Arusha Jesen Mbise aliyejishindia kitita cha shilingi milioni 1/- wakati wa uzinduzi wa droo ya kwanza ya promosheni ya akiba inayojulikana kama ‘Weka amana ushinde’ zaidi ya milioni 20 zitashindaniwa na wateja wa benki hiyo.wapili kushoto ni Msamimamizi wa michezo wa kubahatisha nchini ,Abdallah Hamedi.
Mkurugenzi wa benki ya CBA, Gift Shoko( kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi Promosheni ya ‘Weka amana Ushinde’ ambapo zaidi ya milioni 20 zitashindaniwa na wateja wa benki hiyo. Katikati ni Mkuu wa kitengo cha biashara wa benki hiyo,Mussa Kitambi na msimamizi wa michezo ya kubahati nchini Abdallah Hamedi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad