HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 22 August 2017

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK SHEN AHITIMISHA ZIARA YAKE MKOA WA MJINI MAGHARIBI

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Akijadiliana Jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh Ayoub Mahamud Mohamed  alipofika kutembelea Ujenzi wa barabara ya Kwamata -Kinuni mpaka Kijito upele  inayojengwa na Mkandarasi wa kampuni ya Mecco,Rais akiwa katika ziara yake ya kutembelea maendeleo ya Miradi ya Maendeleo Wilaya ya Magharibi”B” katika Mkoa wa Mjini Magharibi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Wananchi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wa Kinuni na Magogoni leo alipofanya ziara ya kutembelea Ujenzi wa barabara ya Kwamata -Kinuni mpaka Kijito upele inayojengwa na Mkandarasi wa kampuni ya Mecco, katika ziara yake ya kutembelea maendeleo ya Miradi ya maendeleo Wilaya ya Magharibi”B” katika Mkoa wa Mjini Magharibi,(kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZMhe.Haji Omar Kheir na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud
Baadhi ya Wananchi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wa Kinuni na Magogoni wakiwa katika shamra shamra wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani ) alipofika kutembelea Ujenzi wa barabara ya Kwamata -Kinuni mpaka Kijito upele leo inayojengwa na Mkandarasi wa kampuni ya Mecco,Rais akiwa katika ziara yake ya kutembelea maendeleo ya Miradi ya maendeleo Wilaya ya Magharibi”B” katika Mkoa wa Mjini Magharibi
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh Ayoub Mahamud Mohamed Akieleza Machache Namna kampeni ya Mimi na wewe ilivyoweza kuleta Mapinduzi Makubwa Kwenye Wilaya ya Magharibi B Ambapo wamefanikiwa Kujenga Madarasa Matatu na Maabara  kwa Muda wa Siku kumi na Moja,Rais Shein Amempongeza Mkuu waMkoa huyo kwa Juhudi kwabwa Anazojitolea kuwaletea Maendeleoa Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Akiwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko  Fumba wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara  kuangalia ujenzi wa nyumba hizo zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group,(kushoto ) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibu Nd,Ayoub Mohamed Mahmoud.

  
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibu Nd,Ayoub Mohamed Mahmoud Akimkabidhi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Moja ya zawadi zilizotolewa na Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakati wa Majumuisho ya Ziara ya Siku tatu Aliofanya kwenye Mkoa wa Mjini Magharibi Kukagua Shuguli za Maendeleo


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Akiwa Ameambatana na Viongozi Mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar baada ya Kuhitimisha Ziara ya Siku tatu kwenye Mkoa wa Mjini Magharibi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad