HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 3, 2017

WASANII WA BONGOFREVA WAASWA KUZINGATIA MATUMIZI YA LUGHA.

Wasanii wa Bongo Freva  hapa nchini wameaswa kukuzingatia matumizi ya Lunga pamoja na mavazi  ili kuepushafungia fungia ya kazi zao za sanaa hayo yamesemwa leo wakati wa mkutano wa  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe na wasanii wa nyimbo za bongo Freva pamoja na wadau mbalimbali na sanaa hapa nchini jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wasanii wa nyimbo za Bongo Freva hapa nchini kuhusu maswala mbalimbali yanayowahusu wasanii hao, pia wameshauliwa kujiunga kusajili kazi zao pamoja na kulipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kupata miongozo mbali mbali COSOTA pamoja na BASATA.
 Baadhi ya wasanii wa Nyimbo za Bongo Freva  hapanchini kutoka kulia ni Wastara Thomasi, msanii wa Bongo Fleva, Khadija Shaban (Keisha) na Witnes Mwajaga wakiwa katika Mkutano wa wasanii wa Bongo freva na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe jijini Dar es Salaam leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Msanii Witnes Mwajaga akiwa na wasanii wengine wa Bongo Freva  jijini Dar es Salaam leo wakati  wa Mkutano  na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe jijini Dar es Salaam leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea saa ya ukutani ikiwa ni Rambirambi kutoka kwa wasanii wa Mziki wa Bongo Freva  kama pole kufiwa na Mkewe.
KaimuKatibu Mkuu Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Onesmo Kayanda akizungumza na wasanii wa Bongo Freva jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na wasanii hao kuzingatia maadili, kuzingatia matumizi ya Lugha ili kuepusha masuala ya Kufungiwa kazi zao za wasanii hapa nchini.
Baadhi ya wasanii wakisikiliza kwa makini kwenye mkutano na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fisoo akisikiliza kwa makini katika mkutano wa Wasanii wa Bono freva na  
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe jijini Dar es Salaam leo.
 Kushoto ni Mwanasheria, Albert Msando akizungumza na wasanii pamoja na wadau mbalimbali wa sanaa hapa nchini walipokutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe jijini Dar es Salaam leo.
 Kushoto ni Msanii wa Bongo Freva Yesaya Ambwene a.k.a AY akiwa katika mkutano na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe jijini Dar es Salaam leo.
 Afisa Kodi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Sydney Mkamba  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa mkutano wa wasanii  na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe jijini Dar es Salaam leo.
Naibu msajili mkuu wa Wakala wa usajili wa Biashara na leseni (BRELA), Andrew Mkapa akizungumza na wasanii wa Bongo Freva jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na umhimu wasanii hao kujisajili na BRELA.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad