HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 12 August 2017

Wallace Karia, Michael Wambura waibuka kidedea TFF

Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF umehitimishwa kwa aliyekuwa makamu wa Rais wa Shirikisho hilo Wallace Karia kushinda kwa jumla ya kura 95 na kuwabwaga wapinzani wake.

Uchaguzi huo umefanyika leo mkoani Dodoma ukiwa wa amani kwa wajumbe wa mkutano mkuu pamoja na wagombea wenyewe.

Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi wa TFF, Wakili Revocatus Kuuli akitangaza matokeo hayo ambapo alimtangaza Walace Karia kama mshindi wa kinyang'anyiro kwa kura 95 kati ya kura 127, akifuatiwa na Ally Mayay mwenye kura 9 sambamba na Shija Richard.

Kuuli ametangaza kuwa, katika nafasi ya makamu wa Rais, Michael Richard Wambura ameweza kushinda katika nafasi hiyo kwa kura 85.

Kwa upande wa wajumbe wa mkutano mkuu kumekuwa na maingizo mapya kutoka kanda mbalimbali za nchini.

Zone 1: Saloum Chama 
Zone 2: Vedastus Lufano 
Zone 3: Mbasha Matutu 
Zone 4: Sarah Chao 
Zone 5: Issa Bukuku 
Zone 6: Kenneth Pesambili 
Zone 7: Elias Mwanjala 
Zone 8: James Mhagama 
Zone 9: Dunstan Mkundi 
Zone 10: Mohamed Aden 
Zone 11: Francis Ndulane 
Zone 12: Khalid Abdallah 

Zone 13: Lameck Nyambaya
Rais mpya wa Shirikisho la soka nchini (TFF), Walles Karia 
Makamu wa Rais mpya wa Shirikisho la soka nchini (TFF), Michael Wambura .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad