HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 7 August 2017

VIOTA VYA MAKULAJI VYA PIZZA HUT VYAZINDULIWA MLIMANI CITY NA OYSTERBAY JIJINI DAR LEO.

Mkurugenzi Mkuu wa Pizza Hut Afrika, Ewan Devenpot(Katikati) akikata utepe kufungua Mgahawa wa Pizza Hut Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Vikram Desai pamoja na Meneja masoko wa Pizza Hut Tanzania,Bahati Komba.
Mkurugenzi Mkuu wa Pizza Hut Afrika, Ewan Devenpot(Katikati) kwa pamoja wakishangilia mara baada ya kukata  utepe kufungua Mgahawa wa Pizza Hut Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Pizza Hut, Vikram Desai pamoja na Meneja masoko wa Pizza Hut Tanzania,Bahati Komba.
Sehemu husika kwa wahusika watakaotembelea Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Wahudumu Pizza Hut Mlimani City jijini Dar es Salaam wakifanya mambo ya ulaji leo wakati wa uzinduzi wa Kiota cha makulaji Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Pizza Hut, Vikram Desai akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa Ufunguzi wa Mgahawa Piza Hut Mlimani City jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na jinsi watanzania wanavyoajirika katika mgahawa huo.
Amesema kuwa  ajira zilizopo ni katika viwanda vya mabox ambayo nao hutumia katika kuandaa Pizza pamoja na viwanda vya chill source, Tomato source ambapo kuna watu ambao wameajiliwa katika viwanda hivyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Pizza Hut, Vikram Desai na baadhi ya wateja wakionja pizza zilizoandaliwa ikiwa kunapizza za nyama, mbogamboga pamoja na uyoga.
 
Pizza Hut inamilikiwa na kampuni ya Dough Works Ltd, sasa kuajiri wafanyakazi zaidi ya 100 ambao ni watanzania hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Pizza Hut, Vikram Desai wakati wa uzinduzi wa  migahawa miwili iliyopo Mlimani City na Oysterbay jijini Dar es Salaam leo.

akizungumza katika uzinduzi wa migahawa hiyo amesema kuwa Mwaka huu mgahawa wa Pizza Hut ulitambulisha usambazaji bure wa chakula katika ofisi na majumbani na hivyo kuwarahisishia huduma wateja wake.


Migahawa miwili ya Pizza hut ipo katika eneo la maduka la Mkuki, jengo la Peugeot na Shoppers Plaza Mikocheni inaendelea kuhudumia mamia ya wananchi kwa chakula cha mchana na usiku.

Migahawa ya Pizza Hut ni ya kisasa ikiwa na sehemu ya watoto ya michezo mbalimbali, na sehemu za kukaa za ndani na nje. Pamoja na kuwa na chakula kitamu aina ya Pizza pia wametambulisha aina mbali mbali za bidhaa za kuku zenye ladha tofauti.

Zaidi ya mpango huo wa kupanua biashara kwa migahawa miwili zaidi kabla ya mwisho wa mwaka pia tunaangalia uwezekano wa kufungua biashara katika mikoa ya Dodoma, Arusha na Mwanza. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad