HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 7, 2017

VETA YAGUNDUA KIFAA CHA KULAZIMISHA MADEREVA WA PIKIPIKI KUVAA KOFIA NGUMU

Mkuu wa wilaya ya Newala, Aziza Mangosongo, akitembelea banda la VETA katika maonesho ya Kilimo 2017 yanayoendelea mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo ambapo alipongeza VETA kwa kuweka fursa nyingi za mafunzo ya ujuzi kwa makundi mbalimbali ya wananchi. Aliahidi kushirikiana na VETA ilikuwa wezesha wananchi wilaya ni kwake kunufaika pia na fursa mbalimbali za mafunzo ya ufundi stadi.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Medi ya mkoani Mtwara wakipata maelekezo juu ya aina ya mafunzo yanayotolewa katika vyuo vya ufundi Stadi walipotembelea banda la VETA katika Maonyesho ya kilimo ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
.Mwalimu wa Elektroniki wa Veta Kipawa, Aneth Mganga akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda la VETA Pikipiki inayoendeshwa ni lazima dereva awe amevaa kofiangumu.
Wananchi wakipata maelezo ya jiko la mafuta ya taa ambalo limebuniwa kwa kutotumia mafuta mengi na halina moshi.
Baadhi ya wananchi waliofika kutembelea banda la VETA ili kuweza kupata taarifa mbalimbali kuhusianana VETA pamoja na kuaangalia teknolojia mbalimbali.


Na Chalila Kibuda,GlobuyaLindi 

Katika kukabiliana na changamoto za madhara ya ajali za pikipiki yanayosababishwa na madereva kutovaa kofiangumu (helmet), Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imebuni teknolojia ya kukabiliana na hilo. 

Mwalimu wa fani ya elektroniki kutoka VETA Kipawa, AnethMganga, amebuni mfumo wa kielektroniki unaozuia pikipiki kuwa kampaka dereva awe amevaa kofiangumu (helmet). 

Akizungumza na katika viwanja vya maonesho ya Nanenane Ngongo, mkoani Lindi, mwalimu Aneth amesema mfumo huo ukianza kutumika na madereva wa pikipiki utapunguza madhara endapo kunatokea ajali kwa kuwa bila ya kuvaa kofiangumu pikipiki haiwaki na hata ukiwa katika mwendo ikitokea ukavua kofiangumu pikipiki itazimika. 

Aidha, katika usalama barabarani inasaidia kuzuia wizi wa pikipiki kwani mwizi hatoweza kuiwasha bila kofiangumu ambayo imeunganishwa kieletroniki. 

Aneth amesema anaendelea kufanya utafiti nakuboresha zaidi ubunifu huo, lakini ameomba serikali na wadau mbalimbali kuunga mkono ili uweze kuenea, kukubalikana kutumika na waendesha pikipiki katika maeneo mbalimbali nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad