HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 23 August 2017

UAMUZI WA KESI YA MANJI KUJULIKANA IJUMAA AGOSTI,25 MWAKA HUU.

Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuph Manji  akizungumza na
 wakili wake wa utetezi, Hudson Ndusyepo leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kabla ya upande wa utetezi wake kuuliza maswali upande wa Mashtaka.
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, siku ya ijumaa itatoa maamuzi dhidi ya kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili mfanyabiashara maarufu nchini Yusuph Manji kama ana kesi ya kujibu ama la.Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha amesema hayo leo mapema baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi dhidi ya kesi hiyo kwa kuita mashahidi watatu.

Kabla ya uamuzi huo kutolewa, shahidi wa tatu na wa mwisho, Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Domician Dominic (49) ameshindwa kuithibitishia mahakama hiyo kama sampuli ya mkojo alioufanyia uchunguzi ni wa Mfanyabiashara Yusufu Manji au Polisi.

Akijibu swali  wakili wa utetezi, Hudson Ndusyepo la kumtaka, kuieleza mahakama kama anatambua mkojo huo ni wa nani alisema, hatambui kama mkojo ni wa Manji au Polisi kwa kuwa hakuwepo msalani wakati sampuli hiyo inatolewa badala yake yeye alitoa kontena na kumpatia Polisi ili Manji aweke sampuli hiyo ambapo baada ya kuipokea  Kutoka kqa Koplo Sospeter.
Alisajili kontena hilo kwa kuipa namba ya maabara 367/2017.

Ameongeza katika uchunguzi wa awali aliofanya aligundua mkojo huo ulikuwa na kemikali inayoitwa benzodiazepines.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Timon Vitalis, Shahidi huyo amedai mahakamani hapo kuwa kemikali zilizokutwa kwenye mkojo Wa Manji ni dawa ambao hutumika kwa ajili ya kupunguza maumivu makali kwa maelekezo ya daktari na pia kumsaidia mgonjwa kupata usingizi.

Ameongeza, katika hatua ya pili ya uchunguzi aligundua dawa inayoitwa Morphine yenye viashiria vya heroine ambayo wakati mwingine hutumika wakati wa upasuaji.
Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuph Manji  akizungumza na
 wakili wake wa utetezi, Hudson Ndusyepo leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kabla ya upande wa utetezi wake kuuliza maswali upande wa Mashtaka.
 Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuph Manji akielekea kupanda Gari akielekea Mahabusu. Agosti 25 mwaka huu ambayo ni Ijumaa Uamuzi kama  ana kesi ya kujibu au la katika kesi ya dawa za kulevya kujulikana rasmi.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad