HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 2 August 2017

TIMU YA TMT YAIFUATA MCHENGA FAINALI YA SPRITE BBALL KINGS


Nahodha wa timu ya TMT Isihaka Masoud (jezi ya Bluu) akiwania mpira na mchezaji wa timu ya Kurasini Heat Katika mchezo wa tatu wa hatua ya nusu fainali ya Sprite Bball Kings uliomalizika kwa TMT kutoka na ushindi wa alama 99 kwa 71.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


TIMU ya TMT imefanikiwa kuifuata Mchenga katika hatua ya fainali ya mpira wa kikapu ya Michuano ya Sprite Bball Kings baada ya kuiondoa Kurasini Heat kwa alama 99 dhid ya 71.

Mchezo huo uliochezwa jana katika Viwanja vya Don Bosco Oysterbay ulikuwa na ushindani mkubwa sana kwa kila timu ambapo katika nusu fainali ya kwanza na ya pili zilimalizika kwa kila upande kupata ushindi.

Mkurugenzi wa Ufundi na mashindano TBF Manase Zablon amezipongeza timu za Mchenga Bball Stars na TMT kwa kuingia katika hatua ya fainali ya michuano ya Sprite Bball Kings 2017.

Manase amesema kuwa kwa sasa hatua ya fainali inatarajiwa kuwa wiki ijayo na zitachezwa katika hatua ya michezo mitano na watawatangazia ni katika uwanja gani zitachezwa.

Kwa upande wa Nahodha wa timu ya TMT, Isihaka Masoud amesema kuwa mchezo wao dhidi ya Kurasini Heat ulikuwa ni mgumu sana kwani walivyopoteza mchezo wa kwanza waliangalia wapi walipokosea na katika mchezo wa nusu fainali ya pili na ya tatu wamehakikisha wanatoka na ushindi na hilo wamefanikiwa na kuingia fainali.

Isihaka amesema kuwa, haiofii timu ya Mchenga kwani maandalizi mazuri ndiyo yatakayoonekana ndani ya Uwanja ingawa wanafahamu ni timu nzuri yenye wachezaji wazoefu na wazuri.

 Nahodha wa timu ya Kurasini Heat Rajab Hamis ( jezi nyeupe) akijaribu kumtoka mchezaji wa timu yw TMT katika mchezo wa tatu wa hatua ya nusu fainali ya Sprite Bball Kings uliomalizika kwa TMT kutoka na ushindi wa lama 99 kwa 71.
 Piga nikupige langoni mwa timu ya Kurasini Heat Katika mchezo wa tatu wa hatua ya nusu fainali ya Sprite Bball Kings uliomalizika kwa TMT kutoka na ushindi wa alama 99 kwa 71.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad