HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 16 August 2017

StarTimes yazindua msimu wa tatu wa uoneshwaji wa ligi ya Bundesliga 2017/2018

Na Agness Francis, Blogu ya jamii.
Kampuni ya  Startimes Tanzania imezindua uoneshaji wa ligi ya  Bundesliga  mwaka 2017/2018 ambayo itarushwa mubashara kupitia  vipindi vya startimes  kwa wapenzi wa soka hapa  nchini

Uzinduzi huo umefanyika  jijini Dar es Salaam lengo ni kuwa  kuwafahamisha wapenzi  wa mpira kununua ving’amuzi na   kujiunga na vifurushi  ili kuburudika na mechi hizo ambazo ligi hiyo itakuwa ikiionyeshwa moja kwa moja na startimes.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif  amesema kuwa ipo fursa kwa waandishi wa habari za michezo  kufanya mashindano ya  uandishi wa mechi  hiyo na kwa mshindi  wa shindano hilo atagharamiwa safari zote za ti ya ndege  kwenda moja kwa moja Ujerumani.

Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Suluhu nae amesema wana mahusiano mazuri na bundesliga  kwa kuwa na mkataba wa miaka mitano na hadi sasa ni mwaka wa tatu kuonyesha ligi hiyo.

Meneja Uwendeshaji  Startimes, Gaspa Ngowi  amesema kuwa  huduma mpya ya  malipo kwa wale wenye hali ya chini  wanaweza  kulipia siku moja king’amuzi  cha Startimes  kwa gharama ya bei ya shilingi 1000, ambapo kwa wiki utalipia elfu 4000.

Hata hivyo mhariri mkuu wa gazeti la Championi , Salehe Jembe amesema  kuwa  ligi ya Bundesliga  ina ubora na kuburudisha zaidi kulinga na  ligi zingine duniani  kwa kuwa na wachezaji bora 

Nae Meneja mahusiano wa Tabibu TV, Kaki Mwaigomole ametoa shukrani kwa kampuni ya  startimes kwa kuwapa fursa ya kuweza kuonyesha mubashara  mtanange huo ambao utaanza rasmi tarehe  18-27 Agosti mwaka huu
Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa kuonesha ligi ya Bundesliga kwa msimu wa mwaka 2017/18 uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif(wa pili kutoka kushoto) akikata utepe pamoja na wadau mbalimbali wa mpira hapa nchini. 
Baadhi ya wafanyakazi wa StarTimes Tanzania wakfuatilia yaliyokuwa yanajiri kwenye uzinduzi huo
Mtangazaji wa kipindi cha michezo Radio Clouds 'Sports Extra' na Clouds Tv 'Sports Bar', Shaffih Dauda akitoa uchambuzi pamoja na kubashiri ligi hiyo itakavyokuwa kwenye msimu wa mwaka 2017/2018.
 Mhariri mkuu wa gazeti la Championi, Salehe Jembe akitolea ufafanuzi kuhusu ligi ya Bundesliga ya nchini Ujerumani itakavyokuwa kwa msimu wa mwaka 2017/18 kwenye uzinduzi wa kuonesha ligi hiyo kwa mwaka wa tatu kupitia kwenye king’amuzi cha Startames.
 Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Suluhu akizungumza kuhusu kampuni hiyo wanavyoshirikiana kuonesha ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga
Picha ya Pamoja 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad