HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 28, 2017

Shindano la kumtafuta mbunifu chipukizi linaloendeshwa na Swahili Fashion Week laanza

Hayawi hayawi sasa yamekuwa, ile safari ya kusherekea miaka 10 ya mafanikio ya jukwaa kubwa la mitindo Afrika Mashariki na Kati imeanza rasmi.

Kwa miaka 9 maonesho ya Swahili Fashion Week yamebaki kuwa jukwaa kuu kwa Afrika Mashariki katika kuvumbua vipaji vya kipekee na mitindo maarufu ya baadae duniani. Ni ukweli usiopingika kuwa maonesho ya Swahili Fashion Week yana nia na shauku kubwa ya kuwatafuta na kuwakuza wabunifu bora wa baadae, ndio maana  jukwaa la shindano la mbunifu chipukizi lijulikanalo kama Washington Benbella Emerging Designer Competition  lilifikiriwa ili kutoa nafasi kwa wabunifu chipukizi na kuupeleka mbele ubunifu wao.

“Tuna furaha sana kusherekea miaka 10 ya shindano la Washington Benbella Emerging Designer Competition, tumekuwa mashaidi wa mafanikio makubwa ya washindi waliopita sababu tunashauku ya kukuza nyota wa ubunifu. Tumefarijika sana kuanza mashindano haya, katika kukamilisha miaka 10 ya uwepo wa maonesho ya mavazi “Swahili Fashion Week” tunatarajia kuona vitu vizuri Zaidi ya ubunifu wa kawaida, na Zaidi, kila kitu kiwe cha kupendeza.”.

Kila mwaka Ubora na upekee wa mitindo ya washiriki unaendelea kushangaza na kuwavutia watazamaji. Kutokana na dhamira ya maonesho ya mwaka huu ni “ Maadhimisho ya miaka 10 ya Swahili Fashion Week”  hivyo basi  kuna vitu vingi vya kutegemea katika maonesha haya haswa katika shindano hili la mbunifu chipukizi sababu litaonesha mitindo ya washindi wote waliopita.

“tunajitahidi kuvumbua vipaji na kuifanya kazi yao kuwa ya kimataifa, tuna wasihii wabunifu vijana kuchukua nafasi hii adimu kwa umakini na kukusanya kazi zao bora za ubunifu ambazo zitawapatia nafasi ya kuwa kati ya washiriki 10 watakaochaguliwa kuweka historia kwa kuonesha mavazi yao katika maonesho ya  10 ya Swahili Fashion Week mwezi disemba”

Kwa wabunifu chipukizi watakao vutiwa kushiriki kwenye shindano hilo watapata taarifa Zaidi kupitia fomu zetu zilizopo kwenye tovuti yetu ya www.shwahilifashionweek.com, mwisho wa kukusanya fomu hizo ni tarehe 9 Septemba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad