HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 28 August 2017

Morogoro,Mbeya na Kilimanjaro washerehekea miaka 40 ya Safari Lager kwa kishindobi

KAMPUNI ya Bia Tanzania kupitia bia yake ya Safari Lager imesherekea na wateja wake kwa namna tofauti katika kuadhimisha miaka 40 ya Bia ya Safari Lager toka kuanza kuzalishwa kwake hapa nchini tangu mwaka 1977.

 Shamrashamra hizo zilianza rasmi mkoani Morogoro siku ya Ijumaa agosti 25 katika Pub ya Airport iliyopo maeneo ya Airport mjini Morogoro na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa Morogoro waakiburudishwa na Dj kutoka Planet Radio Fm, marufu kwa jina la Andrew B.

Shamrashamra hizo ziliendelea siku ya Jumamosi kwa Mbeya na Moshi-Kilimnajaro, ambapo Moshi ilikuwa funga Mtaa maeneo ya double road ambapo mtaa wa Madina ulifungwa na wakazi wa Moshi huku wakiburudishwa na Dj. Virus huku Mbeya ilifanyika New City Pub na kuhudhuria na mamia ya wakazi wa Mbeya huku wakipata burudani kutoka kwa Dj Nicky.Akizungumzia sherehe hizo Meneja wa bia ya Safari Lager Bi. Edith Bebwa  alisema kuwa hatua ya mafanikio iliyofikiwa na bia ya Safari ni ya kujivunia na hasa kwa sababu bado inaendelea kuwa moja ya kinywaji kinachopendwa zaidi katika soko lenye vinywaji vingi vya aina ya bia.

“Safari Lager ni bia inayoongoza kwa tuzo za ubora wa kimataifa na inaendelea kuwa bia inayopendwa nchini kwasababu ya ubora wa hali ya juu na zaidi hasa kwa sababu ya wateja wetu. Tumeandaa burudani ili kuwashukuru wateja wetu kwa sapoti yao kwa bia yetu hii halisi ya kitanzania.”

Bia ya Safari Lager ni bia yenye miaka mingi katika soko la Tanzania yenye tuzo nyingi za dhahabu ( Gold Monde Selection) na mwaka 2014 Safari lager ilipata tuzo ya hali ya juu ya Monde Selection kwa kuwa bia bia yenye tuzo nyingi za dhahabu za Monde Selection.


 “Tunajivunia kuwa nchini kwa miaka 40 na bado bia ya Safari Lager ikiwa ni chaguo namba moja la Watanzania.
Tunawaalika wateja wetu wote na wapenzi wa Safari Lager waje kusheherekea nasi tutakapokuwa tukija mikoani kama hivi.
aliongezea Edith.

Safari Lager ina mtazamo wa tofauti kwani huzingatia ilikotoka na misingi inayoifanya kuwa imara na kuendelea kusonga mbele na ndiyo maana inasherehekea miaka 40 huku ikitazama mbele kwa kusema #40NABAADO.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad