Kituo cha kurusha matangazo cha Radio Times Fm leo Agosti 07, 2017
kimezindua rasmi msimu wake mpya wa Mapinduzi ya Burudani na kutambulisha
ratiba mpya ya vipindi na Logo mpya yenye muonekano wa rangi ya purple.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mapema hii leo, Msimamizi wa vipindi na
uzalishaji wa Radio Times Fm Amani Missanah amesema kuelekea miaka 18 ya
Times Fm Agosti 28 wameamua kubadili muonekano wa kituo hicho wenye
mlengo wa kuwafikia watanzania wengi zaidi na kuwagusa kwa taarifa za ukweli
na uhakika na burudani isiyo na kifani.
Amesema dhamira ya kubadili muonekano ni pamoja na kuendana na maudhui
ya kituo hicho kwa kuwa wabunifu na watatuzi wa Matatizo ya kijamii kama
ilivyo kawaida ya Times Fm kwa Kupitia Vipindi vyake vilivyoboreshwa zaidi.
“Lengo letu la kubadili muonekano na kutumia rangi ya purple ni kuonesha
Busara iliyonayo Times Fm kwa wasikilizaji ,Heshima, lakini pia Mamlaka.
(Ni
rangi iliyotumiwa na matajiri wengi wakubwa wa kihistoria) lakini pia Wafalme,
mfano Daudi hata pia Yusuph na hata madhabauni pia Inamaanisha utajiri”
Miongoni mwa rangi zingine zilizoanza kutumika ni pamoja na rangi ya Orange
inayohamasisha uchangamfu na kuonesha mtu ambaye yupo optimistic zaidi.
Aidha amesema rangi Nyeupe Inamaanisha usafi, na kumaanisha Neutrality,
pia ni rangi ihamasishayo Ubunifu ndani yake.
Akiongea kupitia kipindi cha Maisha Mseto kinachoongozwa na Stanslaus
Lambart, Florah Matthew na Fredrick Mabula amevitaja vipindi hivyo vya wiki
kuwa ni Maisha Mseto, Mitikisiko ya Pwani ,The PlayList ambayo kwa sasa
itafanyika mchana kuanzia saa nane hadi saa kumi na mbili jioni, Wizara ya
Michezo, Habari Xtra, Campus Vibes na Pillow Talk.
Upande wa vipindi vya wikiendi alisema ni ‘HABA NA HABA, Student Center, Dira
Yetu,Deejays Battle ,Mita Mia,Request Zone,Afro Vibes,Gospel Hits
,Charts,Chipuka,Mambo ya Fedha,Bongo Dot Home,Old schools,Sunday Slowjam.
“Times Fm hivi karibuni inatarajia kuanza kusikika katika mikoa mbali mbali
ikiwemo mikoa ya Dodoma na Mbeya ,pia tunazo frequency za Mikoa mingine
ambayo ni Tanga ,Morogoro,Iringa ,Songea ,Arusha Kilimanjaro na Mwanza
ambapo tunataraji kuanza kusikika hivi punde .
Amewataka wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi kufanya matangazo na Times
Fm kwa punguzo kubwa la bei kwa wafanyabiashara ndogondogo na kubwa na
kutoa fursa ya kutumia gari la kisasa kabisa la kurushia matangazo hapa nchini
Tanzania OB-VAN .
No comments:
Post a Comment